Pata taarifa kuu
HAKI-MAUAJI

Mauaji ya balozi wa Italia nchini DRC: washtakiwa sita wahukumiwa kifungo cha maisha

Wanaume sita wamehukumiwa kifungo cha maisha siku ya Ijumaa huko Kinshasa kwa mauaji ya balozi wa Italia, mlinzi wake na dereva mnamo Februari 2021, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Jeneza la Balozi wa Italia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Luca Attanasio, huko Limbiate, karibu na Milan, Italia, Ijumaa Februari 26, 2021.
Jeneza la Balozi wa Italia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Luca Attanasio, huko Limbiate, karibu na Milan, Italia, Ijumaa Februari 26, 2021. © Claudio Furlan/LaPresse via AP
Matangazo ya kibiashara

Adhabu ya kifo ilikuwa imeombwa na mwendesha mashtaka wa umma, lakini haikuzingatiwa na mahakama ya kijeshi ya Kinshasa-Gombe, ambayo imetoa uamuzi wake.

Upande wa utetezi umeliambia shirika la habari la AFP kwamba utakata rufaa. Kwa hiyo kesi nyingine itasikilizwa mbele ya mahakama ya kijeshi. Wafungwa wa tano kati ya sita wanazuiliwa katika jela la kijeshi la Ndolo, na wa sita yuko mafichoni.

Walishtakiwa kwa "mauaji, kushirikiana na kundi la wahalifu, kumiliki silaha kinyume cha sheria na risasi za vita", walipatikana na hatia ya mauaji mnamo Februari 22, 2021 ya balozi wa Italia nchini DRC, Luca Attanasio, mlinzi wake Vittorio Iacovacci, na dereva wa shirka la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) nchini DRC, Mustapha Milambo.

Watu hao watatu waliuawa kwa kupigwa risasi katika Mbuga ya Kitaifa ya Virunga, katikamkoa wa Kivu Kaskazini (mashariki), eneo lililokumbwa na ghasia kutoka kwa makundi yenye silaha kwa takriban miaka 30.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.