Pata taarifa kuu

Mauaji ya balozi wa Italia nchini DRC: Kesi yaanza kusikilizwa

Wakongo watano, ambao wanakanusha kuhusika na mauaji ya balozi wa Italia nchini DRC, Luca Attanasio, aliyepigwa risasi na kuuawa baada ya kuviziwa, wamefikishwa Jumatano mbele ya mahakama ya kijeshi huko Kinshasa kwa mauaji hayo yaliyotokea 2021 mashariki mwa DRC, kulingana na shirika la habari la AFP.

Luca Attanasio alifariki mnamo Februari 22, 2021 baada ya kupigwa risasi na kujeruhiwa katika eneo lililo kuwa karibu na Hifadhi ya Kitaifa ya Virunga.
Luca Attanasio alifariki mnamo Februari 22, 2021 baada ya kupigwa risasi na kujeruhiwa katika eneo lililo kuwa karibu na Hifadhi ya Kitaifa ya Virunga. REUTERS - YARA NARDI
Matangazo ya kibiashara

Mshtakiwa wa sita, ambaye yuko mafichoni, anahukumiwa bila kuwepo mahakamani na mahakama ya kijeshi katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kesi hii inasikilizwa katika gereza la kijeshi la Ndolo huko Kinshasa, ambapo washitakiwa wanazuiliwa.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa Oktoba 12 lakini ilisitishwa mara moja kwa ombi la mawakili wa upande wa utetezi ambao walitaka kutambuwa yaliyomo kwenye faili za wateja wao.

Kwa mara nyingine, uhalali wa kesi hiyo haujasomwa wakati kesi yenyewe ilianza kusikilizwa tena Jumatano, mmoja wa mawakili Joseph Amzati, ameiomba mahakama ya kijeshi ijitangaze kuwa haina uwezo wa kushughulikia kesi hiyo, kwa misingi hasa kwamba wateja wake walikamatwa huko Goma (Mashariki)mapema 2022, ni raia wa kawaida. Pia alitoa wito wa kuachiliwa kwao kwa muda kwa sababu, aliongeza, "wote wanadai kutokuwa na hatia."

Kwa niaba ya mwendesha mashtaka wa umma, hakimu Luteni-Colonel Joseph Malikidogo alipinga maombi hayo mawili. Washtakiwa hao, alielezea, wako katika kesi ya mauaji, ushirika wa uhalifu na "umiliki haramu wa silaha na risasi za kivita", akibaini kwamba mashitaka dhidi yao ni lazima yashughulikiwe na maakama ya kijeshi. "Mauaji hayo yalifanywa kwa silaha za vita," amesisitiza.

Kuhusu kuachiliwa kwa muda, aliendelea luteni kanali, "Sijui ni nini kitakachohalalisha hilo!". Mashitaka yanayowakabili ni makubwa na "ni yenye uzito usioelezeka", amebainisha, akibaini kwamba "itakuwa kashfa sana ikiwa watu wanaoshtakiwa kwa uhalifu kama huo wataachiliwa".

Kisha mahakama iliahirisha kesi hiyo tena na kupanga kutoa uamuzi wake kuhusu maombi ya utetezi Jumatano ijayo, Oktoba 26.

Washtakiwa hao wakiwa wamesimama mbele ya majaji hawakuzungumza chochote. Walielezwa kupitia mkalimani wa Kiswahili, lugha inayozungumzwa mashariki mwa DRC, maudhui ya kikao hicho, ambacho kilihudhuriwa hasa na balozi wa Italia Alberto Petrangeli.

Mtangulizi wake, Luca Attanasio, 43, alifariki Februari 22, 2021 baada ya kupigwa risasi na kujeruhiwa wakati msafara wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) alimokuwa akisafiria uliposhambuliwa kaskazini mwa Goma, nje kidogo ya Hifadhi ya Taifa ya Virunga, eneo linalookumbwa na ghasia kutoka kwa makundi yenye silaha kwa takriban miaka 30.

Mlinzi wake, raia wa Italia, na raia mwingine wa Italia Vittorio Iacovacci, na dereva raia wa DRC kutoka shirka la WFP, Mustapha Milambo, pia waliuawa.

Januari iliyopita, polisi wa Kongo walitangaza kwamba wamewakamata wahusika wanaodaiwa kuhuika na shambulio hili, "wahalifu" ambao mwanzoni hawakuonekana kuwa na nia ya kumuua balozi huyo, bali kumteka nyara na kudai fidia ya dola milioni moja ili aachiliwe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.