Pata taarifa kuu
USALAMA - MALI

Waasi nchini Mali wautuhumu uongozi wa kijeshi kwa uchokozi

Waasi wa zamani, wameushtumu uongozi wa kijeshi wa Mali kwa uchokozi, baada ya kupaa kwa ndege za kivita katika kambi zao, na kuzua wasiwasi wa maandalizi ya vita.

Kundi la CMA (Picha ya kielelezo)
Kundi la CMA (Picha ya kielelezo) © AFP
Matangazo ya kibiashara

Waasi hao wa kituareg, siku ya Jumatano,  wamelishtumu jeshi kwa kuwachokoza kwa makusudi katika mji wa Kidal, Kaskazini mwa nchi hiyo, hali wanayosema, inatishia kusambaratisha mchakato wa amani.

Licha ya shutuma hizo, uongozi wa Mali haujazungumzia suala hilo.

Kundi hilo limetoa malalamishi hayo, wakati likiadhimisha miaka 11 baada ya kuchukua udhibiti wa miji ya Kaskazini mwa Mali, kabla ya kusaini mkataba wa amani na uongozi wa Bamako.

Mwezi Desemba mwaka uliopita, pamoja na makundi mengine, kundi hilo lilitangaza kujiondoa kwenye utekelezwaji wa mkataba wa amani, kwa kile ilichosema kuwa uongozi wa Bamako, hauonyeshi utashi wa kisiasa.

Tangu mwezi Agosti mwaka 2020, Mali imekuwa ikiongozwa na wanajeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.