Pata taarifa kuu

Tiger: Eritrea yakanusha 'madai' ya uhalifu yaliyotolewa na Marekani dhidi yake

Eritrea imeelezea Jumanne kama 'fedheha' na 'yasiyo na msingi' mashtaka ya 'uhalifu wa kivita' na 'uhalifu dhidi ya binadamu' uliyofanywa kulingana na Washington na jeshi lake katika kipindi cha miaka miwili ya migogoro katika jimbo la Ethiopia la Tiger.

Rais wa Eritrea Issaias Afwerki na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed huko Asmara, Eritrea, Julai 9, 2018.
Rais wa Eritrea Issaias Afwerki na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed huko Asmara, Eritrea, Julai 9, 2018. Twitter/ Fitsum Arega
Matangazo ya kibiashara

Madai hayo, ambayo sio mapya, hayategemei ushahidi wowote wa kweli na usioweza kutekelezwa," imesema Wizara ya Mambo ya nje ya Eritrea,kuhusiana na madai hayo yaliyotolewa siku moja kabla na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken.

Shutma hizi "zinaonyesha mwendelezo wa uhasama usio na msingi na uadui ambao utawala wa Marekani unaendelea kuonyesha Eritrea tangu 2009 ili kukuza miundo yake ya kisiasa iliyofichwa," Asmara imesema.

Siku ya Jumatatu jioni, Antony Blinken alishutumu washirika wote wa mzozo huko Tigray ikiwa ni pamoja na vikosi vinavyounga mkono serikali ya Ethiopia na waasi wa kufanya uhalifu wa kivita, akibaini kwamba uhalifu huo 'hukufanywa kwa bahati mbaya' au 'ni madhara ya moja kwa moja ya vita' lakini "ulipangwa na ulifanywa kwa makusudi'.

Lakini pia alishutumu hasa Jeshi la Shirikisho la Ethiopia na washirika wake, jeshi la Eritrea na wanamgambo wa mkoa wa Amhara kwa uhalifu dhidi ya binadamu ikiwa ni pamoja na "mauaji, ubakaji na aina zingine za ukatili wa kijinsia na mateso" bila kutaja vikosi vya waasi vya Tigray.

Utawala wa Eritrea ulisaidia kijeshi serikali ya shirikisho ya Ethiopia ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed kwa kupeleka wanajeshi katika jimo la Tigray kupambana na vikosi vya ukombozi vya raia wa Tigray (TPLF), chama ambacho kilikuwa kikitawala katika jimbo hilo na kufarakiana na serikali ya Ethiopia.

TPLF, ambayo ilitawala Ethiopia kwa karibu miongo mitatu hadi kufika madarakani kwa Bw Abiy mnamo 2018, ni adui mkuu wa Asmara tangu vita kati ya nchi hizo mbili kati ya mwaka 1998 na 2000. "Vita vikali" katika jimbo la Tigray vilisababishwa na  waasi wa TPLF, ambao " walifanya uhalifu mwingi ambapo wangeweza kushtumiwa lakini wamefutiwa uhalifu huo kwa makusudi" na Washington, Asmara imsema.

Serikali ya Eritrea pia inabaini kuwa madai ya Marekani yanatokea wakati sera za nchi hiyo "zinapingwa ulimwenguni kote na hasa barani Afrika". Addis Abeba na Asmara walikataa ushiriki wowote wa Eritrea huko Tigray kwa miezi kadhaa. Mnamo mwezi Machi 2021, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed mwishowe alikiri uwepo wa jeshi la Eritrea.

Washington iliweka vikwazo dhidi ya chama tawala huko Eritrea na jeshi la Eritrea mwishoni mwa mwaka wa 2021, askari ambao walishutumiwa kwa dhuluma nyingi wakati wote wa mzozo, makubaliano ya amani yalitiwa saini mnamo mwezi Novemba 2022 kati ya serikali ya Ethiopia na waasi wa Tigray, lakini Eritrea haijashiriki katika mazungumzo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.