Pata taarifa kuu

Tigray: Blinken ashutumu Ethiopia, Eritrea na waasi kwa kufanya 'uhalifu wa kivita'

Marekani imeamua kwamba wanajeshi wa Ethiopia na Eritrea, pamoja na waasi wa Tigray, walifanya uhalifu wa kivita wakati wa miaka miwili ya vita vya umwagaji damu katika eneo la Tigray nchini Ethiopia, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amesema siku ya Jumatatu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akiwa na Waziri wa Fedha wa Ethiopia Ahmed Shide kwenye bohari ya Umoja wa Mataifa mjini Addis Ababa Machi 15, 2023.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akiwa na Waziri wa Fedha wa Ethiopia Ahmed Shide kwenye bohari ya Umoja wa Mataifa mjini Addis Ababa Machi 15, 2023. © Tiksa Negeri / Pool via AP
Matangazo ya kibiashara

"Tunaziomba serikali za Ethiopia na Eritrea, pamoja na TPLF (vuguvugu la waasi la Tigray People's Liberation Front) kuwawajibisha wale waliohusika na ukatili huu," amesema waziri wa mambo ya nje wa Marekani mbele ya waandishi wa habari, siku chache baada ya ziara yake Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia. "Nyingi ya vitendo hivi havikuwa vya kubahatisha au matokeo ya vita. Vilihesabiwa na kufanywa kwa makusudi", amesema waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani mbele ya waandishi wa habari, siku chache baada ya ziara yake mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia.

Amesema Wizara ya Mambo ya Nje ilifanya "uchunguzi wa kina wa sheria na ukweli" na kuhitimisha kuwa uhalifu huu wa kivita ulifanywa na pande zote zinazohusika, ikiwa ni pamoja na vikosi kutoka eneo jirani.'Amhara. "Tunaziomba serikali za Ethiopia na Eritrea, pamoja na TPLF (vuguvugu la waasi la Tigray People's Liberation Front) kuwawajibisha wale waliohusika na ukatili huu," amesema.

"Mgogoro wa kaskazini mwa Ethiopia umekuwa mbaya sana. Wanaume, wanawake na watoto wameuawa. Wanawake na wasichana wamefanyiwa unyanyasaji wa kijinsia ambao haujawahi kushuhudiwa. Maelfu ya watu wamelazimika kuyahama makazi yao. Jamii nzima imelengwa kwa sababu ya makabila yao. ” ameongeza.

Idadi kamili ni ngumu kutathmini, lakini Marekani inakadiria kuwa watu wapatao 500,000 walikufa wakati wa mzozo huu. Wakati wa ziara yake nchini Ethiopia wiki jana, Bw. Blinken hakutaja kwa uwazi uhalifu wa kivita au uhalifu dhidi ya binadamu, huku akitoa wito wa "maridhiano na uanzishwaji wa majukumu" katika ukatili wa mzozo wa Tigray. Alikutana na Waziri Mkuu Abiy Ahmed, kisha na wawakilishi wa mamlaka ya waasi wa eneo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia.

Pande hizo mbili zimeahidi kutekeleza makubaliano ya amani yaliyotiwa saini Novemba 2 huko Pretoria, ambayo yalimaliza miaka miwili ya mzozo mbaya, alibaini wakati huo wa ziara yake nchini Ethiopia. Alipoulizwa kwa nini hakufanya uamuzi huo alipokuwa nchini Ethiopia, Blnken amesema ilikuwa "inafaa" kufanya hivyo wakati ripoti ya mwaka ya Wizara ya Mambo ya Nje ya haki za binadamu imetolewa siku ya Jumatatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.