Pata taarifa kuu

Afrika Kusini: Malema asema mgomo wa siku ya Jumatatu ulifanikiwa

NAIROBI – Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Afrika Kusini, The Economic Freedom Fighters, Julius Malema, amesema mgomo walioufanya hapo jana nchi nzima, ulifanikiwa kufikia lengo na kutuma ujumbe kwa Serikali ya rais Cyril Ramaphosa.

Julius Malema, Kiongozi wa chama cha  upinzani EFF nchini Afrika Kusini.
Julius Malema, Kiongozi wa chama cha upinzani EFF nchini Afrika Kusini. REUTERS/Siphiwe Sibek
Matangazo ya kibiashara

Malema akionya kuhusu mpango wa Serikali kutaka kubinafsisha shirika la umeme la nchik hiyo, ESCOM.

“Hebu miundo mbinu ilioko itazamwe vizuri itengenezwe kuhakikisha inazalisha umeme wa kutosha.”ameeleza Julius Malema.

00:22

Julius Malerma, Kiongozi wa upinzani nchini Afrika Kusini

Maelfu ya waandamanaji walikusanyika katika mji mkuu Pretoria wakijiandaa kuandamana hadi kwenye Majengo ya Muungano, makao makuu ya serikali, ambapo polisi na wanajeshi walikuwa wakishika doria. 

Raia wengine walikusanyika katika maeneo mengine ya nchi, kulingana na picha kwenye vyombo vya habari vya ndani na kwenye mitandao ya kijamii. 

Kwa mujibu wa maofisa wa polisi nchini Afrika Kusini karibia waaandamanaji wanane walikamatwa usiku wa kuamkia leo Jumatatu kwa kuhusishwa na ghasia. 

Chama cha Economic Freedom Fighters (EFF), chama cha tatu kwa ukubwa nchini humo, kimetoa wito wa kufanyika kwa mgomo na maandamano, na hivyo kuzua hofu ya kurudiwa kwa machafuko ambayo yalisababisha vifo vya miaka miwili iliyopita. 

Mtu mmoja aliripotiwa kufariki wakati wa maandamano hayo ya siku ya Jumatatu katika eneo la Casamance, kusini mwa Senegal,wakati wa  makabiliano kati ya wafuasi wa  Ousmane Sonko na polisi.

 

Tangu Machi tarehe 16, siku ya kuanza kwa kesi ya Sonko aliyeshtakiwa kwa kashfa na Waziri wa Utalii Mame Mbaye Niang, makabiliano yameripoitwa kati ya makundi ya vijana na vikosi vya usalama katika miji kadhaa nchini. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Machi 30.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.