Pata taarifa kuu

Ajali ya feri nchini Gabon: Idadi ya waliofariki yafikia 24

Idadi ya waliofariki baada ya kuzama kwa feri ndogo katika pwani ya Gabon imefikia 24, uratibu wa shughuli za uokoaji umetangaza hivi punde siku ya Jumapili.

Jamaa na marafiki wakiweka mishumaa na maua kwa wale waliopotea kufuatia kuzama kwa feri ndogo, hapa ni katika bandari ya Libreville mnamo Machi 13, 2023.
Jamaa na marafiki wakiweka mishumaa na maua kwa wale waliopotea kufuatia kuzama kwa feri ndogo, hapa ni katika bandari ya Libreville mnamo Machi 13, 2023. AFP - STEEVE JORDAN
Matangazo ya kibiashara

 

Kwa jumla, abiria 124 kati ya 161 na wafanyakazi wa feri hi ndogo, Esther Miracle, iliyokuwa ikibeba abiria na mizigo iliyozama Machi 9 katikati ya usiku karibu na pwani ya Gabon, waliokolewa.

Miili miwili iligunduliwa siku ya Jumapili, mamlaka imesema, na nyingine siku moja kabla, huku zoezi la kutafuta  likiendelea kujaribu kuwapata miili 13 iliyoliosalia 13 ambayo haijapatikana, hususa katika sehemu zingine za feri hii.

"Feri hiyo imepekuliwa kwa asilimia 60, hata hivyo baadhi ya vyumba bado havifikiki kutokana na kuzuiwa kwa njia za kuingia na fanicha", ametangaza Luteni Kanali Joseph Ndjoumigui kwenye televisheni ya taifa.

Siku ya Ijumaa, mwendesha mashtaka wa umma, André Patrick Roponat, alitangaza kuwa watu 33 wamekamatwa tangu kufunguliwa kwa uchunguzi, wakiwemo wajumbe wa Wizara ya Uchukuzi, jeshi la wanamaji na kampuni inayomiliki feri hiyo.

"Kuna uzembe mwingi, maelewano, mapendeleo na mipango midogo," Waziri Mkuu Alain-Claude Bilie-By-Nze alisema siku ya Ijumaa katika ujumbe uliotumwa kwa maafisa kutoka Wizara ya Uchukuzi na Wanamaji.

Siku moja kabla, Waziri wa Uchukuzi wa Gabon, Brice Paillat, alikabidhi barua yake ya kujiuzulu kwa Rais wa Jamhuri, Ali Bongo Ondimba, ambaye alikubali.

Feri hii Esther Miracle, ambayo ni ya kampuni binafsi, Royal Cost Marine (RCM), na ambayo tarehe iliyotengeezwa haijajulikana, ilinunuliwa na shughuli zake kuzinduliwa mnamo mwezi Novemba. Ilikuwa iifanya safari zake kati ya mji mkuu wa Gabon Libreville na bandari ya mafuta ya Port-Gentil.

Ajali hiyo ya feri ilitokea kilomita 10 kutoka pwani na sio mbali na mlango wa ghuba karibu na Libreville, mji mkuu wa Gabon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.