Pata taarifa kuu
USALAMA-BAHARINI

Ajali ya feri nchini Gabon: Idadi ya waliofariki yaongezeka

Idadi ya awali ya watu waliofariki baada ya feri ndogo kuzama nchini Gabon siku ya Alhamisi ya wiki iliyopita imeongezeka hadi sita na 31 hawajulikani walipo baada ya kupatikana kwa miili mitatu mipya, na operesheni ya kutafuta miili mingine inaendelea, serikali imetangaza leo Jumatatu.

Katika bandari ya Môle, mishumaa na picha za wahanga na watu waliokosekana baada ya kuzama kwa feri ndogo "Esther Miracle", kaktika pwani ya Nyonié, nchini Gabon.
Katika bandari ya Môle, mishumaa na picha za wahanga na watu waliokosekana baada ya kuzama kwa feri ndogo "Esther Miracle", kaktika pwani ya Nyonié, nchini Gabon. © Yves-Laurent Goma/RFI
Matangazo ya kibiashara

Miili ya watu watatu ilipatikana Jumapili, serikali imesema kwenye ukurasa wake wa Facebook, zaidi ya siku nne baada ya Esther Miracle, feri ya abiria na mizigo iliyokuwa ikisafiri Libreville na bandari ya mafuta ya Port-Gentil, kuzama katikati usiku.

Kwa hiyo idadi ya waliofariki akiwemo mtoto mmoja imeongezeka kutoka watu watatu hadi sita, na waliokusekana kutoka 34 hadi 31. Kwa wakati huu, watu 124 wamepatikana wakiwa hai tangu Alhamisi kati ya abiria 161 na wafanyakazi walioorodheshwa rasmi na mamlaka.

Meli na wapiga mbizi wanajaribu kutafuta miili mingine. Hatutasitisha zoezi hili hadi tupate miili mingine na hatuna uhakika kuwa tumeopoa miili yote", Waziri Mkuu Alain-Claude Bilie-By-Nze alisema siku ya Jumapili adhuhuri. Serikali haikusema Jumatatu ikiwa feri hiyo iliweza kupatikana.

Siku ya Alhamisi, mwendesha mashtaka wa umma wa Libreville, André Patrick Roponat, aliliambia shirika la habari la AFP kwamba uchunguzi wa jinai umefunguliwa mara moja ili kujaribu kubaini sababu za kuzama kwa feri hiyo. Ikiwa ni hitilafu ya urambazaji au uharibifu, "mmiliki atalazimika kujibu kwa kuhatarisha maisha ya abiria", alisisitiza Bw. Roponat. Lakini kuzama huko kunaweza pia kusababishwa na "mambo mengine ambayo yako juu ya uwezo wa  mtu yeyote", aliongeza. Bahari ilikuwa shwari usiku kucha kuanzia Alhamisi hadi Ijumaa.

feri hiyo, ambayo tarehe yake ya ujenzi haijajulikana, ilinunuliwa na kuzinduliwa kwa njia hii mwezi Novemba mwaka jana. Ni mali ya kampuni ya kibinafsi, Royal Cost Marine (RCM).

Idadi kubwa ya walionusurika waliokolewa siku ya Alhamisi alfajiri alfajiri, hasa kutokana na uingiliaji kati wa mitumbwi ya kibinafsi, wavuvi au atu wengine, meli kutoka kwa kampuni ya kibinafsi ya mafuta na meli ya doria kutoka kwa Jeshi la Wanamaji la Ufaransa. feri hiyo ilizama muda mfupi kabla ya saa kumi usiku, kulingana na serikali. Ajali hiyo ilitokea karibu na pwani, kwenye mlango wa ghuba ambayo inahifadhi Libreville, mji mkuu wa jimbo hili dogo la Afrika ya Kati lenye utajiri wa hidrokaboni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.