Pata taarifa kuu

Wawili wafariki, 28 hawajulikani walipo katika ajali ya feri ndogo nchini Gabon

Kuzama kwa feri ndogo usiku wa Jumatano kuamkia leo Alhamisi nchini Gabon kumesababisha "angalau watu wawili kufariki na watu 28 hawajulikani walipo", afisa wa mamlaka ya bandari ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Alhamisi. Feri hiyo ilikuwa inatokea Libreville kuelekea Port-Gentil.

Ufukwe huko Gabon, karibu na Port-Gentil.
Ufukwe huko Gabon, karibu na Port-Gentil. AFP/Justin Tallis
Matangazo ya kibiashara

Kuzama kwa feri nchini Gabon, iliyokuwa ikitokea Libreville kuelekea Port-Gentil, kumesababisha vifo vya watu wawili na wengine 28 kupotea usiku waJumatano kuamkia leoAlhamisi.

Baada ya kuanza safari, "wahudumu waliripoti kuvuja kwa feri hiyo kati ya saa tisa usiku na saa kumi Alfajiri," kampuni ya Royal Cost Marine imesema leo Alhamisi asubuhi kwenye ukurasa wake wa Facebook. "Hali hii ilisababisha kupotea kwa mawasiliano ya bandari na dereva wa feri. Mamlaka imetahadharishwa na huduma za dharura ziko eneo la tukio, abiria wamekuwa wakiokolewa," kampuni hiyo imehakikisha.

Watu wa kwanza walionusurika wamewasili mapema asubuhi wakiwa kwenye mitumbwi. feri hiyo ilikuwa inabeba abiria 151, kulingana na afisa wa mamlaka ya bandari ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Mara tu wanapowasili, walionusurika hupelekwa moja kwa moja kwenye magari ya kubebea wagonjwa ili kupokea huduma ya kwanza huku hema kubwa likiwa limewekwa kwa ajili ya mapokezi, amebainisha mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP.Β 

Waziri Mkuu, Alain-Claude Bilie-By-Nze, na Waziri wa Mambo ya Ndani, Lambert NoΓ«l Matha, wamezuru eneo la tukio saa sita mchana.Β 

Manusura wengine pia walishuka kutoka kwenye meli ya kampuni ya usafirishaji wa mafuta ya Peschaud ambayo ilishiriki katika uokoaji, kwa kupiga makofi na vilio vya furaha. Wakitembea kwa miguu, baadhi ya abiria walikusanyika na kupiga magoti karibu na bandari, viganja vikielekezwa angani, kabla ya kuimba nyimbo za kidini na kumshukuru Mungu, amebainisha mwandishi wa habari wa AFP.

β€œMungu, Bwana, ulituokoa na maji, tutatoa dhabihu kwa ajili yako, asante Bwana,” alipaza sauti mmoja wa walionusurika katikati ya wengine akiomba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.