Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Macron aanza ziara yake Afrika ya Kati

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anaanza ziara ya siku nne katika ukanda wa Afrika ya Kati mjini Libreville, nchini Gabon, siku ya Jumatano, fursa ya kujionea "uhusiano mpya" anaotaka kuwepo na bara ambalo ushawishi wa Ufaransa unaendelea kupungua.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajiwa nchini Gabon.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajiwa nchini Gabon. REUTERS/Robert Pratta
Matangazo ya kibiashara

Rais Emmanuel Macron anatarajiwa katika mji mkuu wa Gabon, Libreville alasiri, hatua ya kwanza ya ziara ambayo itampeleka Angola, Kongo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Anafanya ziara yake ya kumi na nane barani Afrika tangu kuanza kwa muhula wake wa kwanza wa miaka mitano mnamo 2017. Ziara hii inakuja siku mbili baada ya kutangaza akiwa Paris, mkakati wake wa Kiafrika kwa miaka minne ijayo.

Akizingatia kuongezeka kwa chuki dhidi ya Ufaransa, Emmanuel Macron alitoa wito siku ya Jumatatu "kujenga uhusiano mpya, wenye usawa, wa kuheshimiana na wa kuwajibika" na Afrika. Pia alitangaza kupunguzwa kwa uwepo wa jeshi la Ufaransa, lililopambana dhidi ya wanajihadi kwa miaka kumi katika ukanda wa Sahel.

"Afrika si eneo la mashindano", alisema rais wa Ufaransa, akitetea "mkao wa staha na kusikiliza" katika upanuzi wa hotuba yake huko Ouagadougou mnamo Novemba 2017.

Demokrasia kwanza

Tangu Agosti 2022, jeshi la Ufaransa lilitakiwa kuondoka Mali na Burkina Faso na watawala wa kijeshi katika nchi hizi mbili. Pia liliondoka Jamhuri ya Afrika ya Kati mwezi Desemba ambako iliingilia kati kukomesha ghasia kati ya makabila.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.