Pata taarifa kuu

Emmanuel Macron: Afrika haipaswi kuwa 'nyuma' au uwanja wa 'mashindano'

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza Jumatatu hii, Februari 27, 2023 katika Ikulu ya Elysee mielekeo ya sera yake ya Kiafrika kwa miaka ijayo, kabla ya ziara yake nchini Gabon, Angola, Kongo na DRC, iliyopangwa kuanzia Machi 1 hadi 5.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atangaza mielekeo sera yake ya Afrika mnamo Februari 27, 2023, kabla ya ziara yake katika ukanda wa Afrika ya Kati.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atangaza mielekeo sera yake ya Afrika mnamo Februari 27, 2023, kabla ya ziara yake katika ukanda wa Afrika ya Kati. AFP - STEFANO RELLANDINI
Matangazo ya kibiashara

Mwanzoni mwa hotuba yake, Emmanuel Macron ametaka kuangazia "mtazamo wake wa kina katika kukabiliana na kile kinachotokea katika bara la Afrika", muktadha ambao anaelezea kama "hali isiyo na mfano katika historia", na "jumla ya changamoto zinazosumbua.

"Kutoka kwa changamoto ya usalama wa tabia nchi hadi changamoto ya idadi ya watu na vijana wanaowasili na ambao inatakiwa kutoa mustakabali wa kila moja ya nchi za Kiafrika", lazima "kuunganisha serikali na tawala, kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika elimu, afya , ajira, mafunzo, mpito wa nishati,” amesemarais wa Ufaransa.

Baadaye rais ametangaza "sheria ya mfumo" wa "marejesho mapya" ya kazi za sanaa "kwa manufaa ya nchi za Kiafrika zinazoomba".

"Itapendekezwa katika wiki zijazo na Waziri wa Utamaduni kwa Bunge letu" na "itawezesha kuweka mbinu na vigezo vya kuendelea" na marejesho haya, "kwa kuzingatia ushirikiano wa kitamaduni na kisayansi wa kupokea na kuhifadhi kazi hizi".

Rais wa Ufaransa anatamani "kwamba mbinu hii inaweza kuwa sehemu ya nguvu pana na pia nguvu ya Ulaya".

Na katika mantiki ya kukataa kuipunguza Afrika kuwa "uwanja wa ushindani", akipendelea uhusiano wenye "usawa" kulingana na maneno yake, Bwana Macron ametangaza kwamba Ufaransa katika siku zijazo itakuwa na kambi za kijeshi tu zitakazosimamiwa na nchi husika katika bara hilo. Hii itapelekea "kupunguzwa" kwa idadi ya wanajeshi wa Ufaransa waliotumwa Afrika, lakini "juhudi zitaogezwa" katika suala la mafunzo na vifaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.