Pata taarifa kuu
UCHUNGUZI-USALAMA

Gabon: Waziri wa Uchukuzi ajiuzulu wiki moja baada ya feri 'Esther Miracle' kuzama

Nchini Gabon, wiki moja baada ya kuzama kwa feri ya "Esther Miracle", ambayo iliua takriban watu 21, Waziri wa Uchukuzi amejiuzulu Alhamisi Machi 16. Katika taarifa kwa vyombo vya habari, ofisi ya rais ilionyesha kwamba Brice Paillat "aliwasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Rais wa Jamhuri" Ali Bongo Ondimba, "ambaye amekubali".

Ndugu na marafiki wakiweka mishumaa na maua kwa wale waliofariki kufuatia kuzama kwa feri, kwenye bandari ya Libreville, Machi 13, 2023.
Ndugu na marafiki wakiweka mishumaa na maua kwa wale waliofariki kufuatia kuzama kwa feri, kwenye bandari ya Libreville, Machi 13, 2023. AFP - STEEVE JORDAN
Matangazo ya kibiashara

Taarifa kwa vyombo vya habari, hata hivyo, haijabainisha sababu za kujiuzulu, wala haizungumzii tukio linalohusaiana na feri kuzama. Fericha ya "Esther Miracle" ilikuwa ikifanya safari kutoka mji mkuu wa Gabon Libreville na bandari ya mafuta ya Port-Gentil ilipozama mnamo Machi 9 katikati ya usiku takriban kilomita kumi kutoka pwani.

Maafisa wanne wa utawala wa Jeshi la Wanamaji na Masuala ya Baharini wamesimamishwa kazi. Shughuli za mmiliki wa meli, mmiliki wa feri zilisimama hadi tagazo nliingine. Kuzuiliwa kwa Maafisa wa polisi na maafisa wa kampuni inayomiliki feri hiyo kunaendelea.

Vikwazo vya siku za hivi majuzi havijatosha kutuliza hasira za familia za waathiriwa wa ajali hiyo. Na kwa ujumla Wagabon - mashirika ya kiraia, upinzani - ambao walidai kujiuzulu kwa Waziri wa Uchukuzi. Na waliohusika na mkasa huu waadhibiwe vikali.

Makosa yalifanyika. Watu walionusurika katika ajali hiyo ya feri walieleza kuwa hawakuongozwa na wafanyakazi hao wakati wa uokoaji, kwani walikaa majini kwa saa nyingi, waking’ang’ania boti zinazoweza kupenyeza maji ambazo zilikuwa zikisafiri kwenye maji hayo.

Uchakavu wa feri hiyo - ambayo tarehe ya ujenzi wake haijajulikana - pia imetiliwa shaka, pamoja na kutofaa kwake kubeba abiria. Ni chombo cha mchanganyiko pia kinachobeba mizigo.

Uchunguzi wa kiutawala na mahakama umefunguliwa, lakini hakuna kilichovuja, na hivyo kuchochea hasira ya Wagabon.

Wakati huo huo, ni Mjumbe wa Waziri wa Uchukuzi ambaye "atahakikisha kushughulikia mambo ya sasa hadi uteuzi wa waziri mpya", inabainisha taarifa kwa vyombo vya habari kutoka ofisi ya rais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.