Pata taarifa kuu
ULINZI-USALAMA

CI: Mazoezi ya kijeshi ya Flintlock 2023 kwa ajili ya mapambano dhidi ya ugaidi yakamilika

Kwa muda wa wiki mbili, wanajeshi 1,300 kutoka nchi 29 walipata mafunzo nchini Ghana na Côte d'Ivoire ili kupambana vyema na tishio la ugaidi. Mafunzo haya yaliandaliwa hasa na operesheni maalum ya Kamandi ya Marekani barani Afrika (US Africa Command).

Mazoezi ya Flintlock, huko Jacqueville, Côte d'Ivoire, Machi 2023.
Mazoezi ya Flintlock, huko Jacqueville, Côte d'Ivoire, Machi 2023. © Bineta Diagne/RFI
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu maalum huko Jacqueville, Bineta Diagne

Makundi mawili yenye silaha yalikutana katika jengo lililotelekezwa katikati ya msitu. Baada ya muda mfupi, vikosi vya silaha vilionekana na kuingia ndani ya jengo hili. Lengo lao: kukamata shabaha zinazochukuliwa kuwa za "thamani ya juu", bila kuwaua. Wote katika mazingira ya uhasama. Meja Nick, simamia mafunzo haya.

Kwa muda wa wiki mbili, askari walipata mafunzo hasa kuhusiana na kukusanya na kuchambua habari. Zoezi hili linaandaliwa mara kwa mara tangu 2005. Kwa mujibu wa Mkuu wa majeshi ya Côte d'Ivoire, Jenerali Lassina Doumbia, hii inafanya uwezekano wa kukabiliana na tishio la makundi ya kigaidi yenye silaha.

"Inatuwezesha kutarajia mabadiliko katika matukio haya. Makundi ya kigaidi yenye silaha hubadilika katika mbinu zao, kwa hivyo tunahitaji kuwa na uwezo unaosasishwa kila mara. Na kufanya hivyo, ni kupeana uzoefu, ujuzi na vitengo vingine, hali ambayo itaruhusu vitengo vyetu maalum kusasishwa. »

Mbali na mbinu za kupambana na vitisho, changamoto pia ni "kuwalinda raia", alibaini Jessica Davis Ba, balozi wa Marekani nchini Côte d'Ivoire, mwishoni mwa mafunzo haya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.