Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Sudan: Marekani yapinga kuachiliwa kwa gaidi aliyemuua Mmarekani mwaka wa 2008

Marekani ilionyesha hasira yake dhidi ya Sudan mnamo Februari 1, 2023. Washington ilimwitisha balozi wa Sudan kufuatia kuachiliwa huru Januari 30 kwa gaidi aliyehukumiwa kifo. Abdel Ra'uf Abuzaid alikuwa amehukumiwa kwa kuhusika kwake katika shambulio lililomuua Mmarekani John Granville na dereva wake, ambaye alikuwa akifanya kazi katika shirika la USAID, mwaka 2008.

Ned Price, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, amelaani kuachiliwa kwa Msudan Abdel Ra'uf Abuzaid.
Ned Price, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, amelaani kuachiliwa kwa Msudan Abdel Ra'uf Abuzaid. AFP - MANUEL BALCE CENETA
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya Juu ya Sudan ilimwachilia huru Abdel Ra'uf Abuzaid mnamo Januari 30, 2023. Na Marekani imeelezea hasirake kufuatia uamuzi huo wa mahakama . Katika majibu yake ya kwanza, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, imesema "imesikitishwa na ukosefu wa uwazi uliosababisha uamuzi huu", pia ikiomba "ufafanuzi" kutoka Sudan.

Lakini jana usiku, msemaji wa diplomasia ya Marekani, Ned Price, alienda mbali zaidi: “Tunalaani vikali kuachiliwa huku kwa upande mmoja. Tunatoa wito kwa serikali ya Sudan kutumia njia zote za kisheria kubadili uamuzi huu na kumkamata tena Abdel Ra'uf Abuzaid. Tunaendelea kutaka ahukumiwe kikamilifu kwa mauaji haya."

Ned Price ameongeza: “Leo tunamwitisa balozi wa Sudan nchini Marekani. Zaidi ya hayo, Balozi wetu nchini Sudan, John Godfrey, amewasiliana na mamlaka za juu zaidi za Sudan, na Naibu waziri wetu Peter Lord atakuwa Khartoum wiki ijayo, ambako atadai hatua kuhusu suala hili nyeti sana. Hatutakubali kushindwa."

Washukiwa wengine wawili bado  wako mafichoni

Kulingana na familia ya gaidi huyo, majaji walishauriana na Wizara ya Mambo ya Nje. Inasemekana Khartoum iliamua kumwachilia huru kufuatia makubaliano ya nchi mbili ya mwaka 2020 ambayo yalitoa fidia ya kulipwa na Sudan kutokana na vitendo vya kigaidi vilivyopita, ikiwa ni pamoja na mauaji ya John Granville.

"Wasudan wanadai kuwa familia ya John Graville imesamehe lakini ni uongo, amejibu Ned Price. Zaidi ya hayo, makubaliano ya nchi mbili ya 2020 hayakuhusu kufungwa au kuhukumiwa kwa Abuzaid. Tumelizungumzia suala hili kwa nguvu zote na viongozi wa Sudani ili kuhakikisha kwamba haki inatendeka. Mhusika wa shambulio hili la kutisha la kigaidi anapaswa kubaki gerezani."

Miaka 15 baada ya shambulio hilo, faili iko mbali na kufungwa kwani washukiwa wengine wawili bado wako mafichoni. Marekani inatoa zawadi ya dola milioni 5 kwa taarifa yoyote itakayosaidia kukamatwa au kupatikana kwa watu hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.