Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-ULINZI

Sudan na Chad zataka kuimarisha usalama katika mpaka wao wa pamoja

Rais wa mpito wa Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, na mwenzake wa Chad, Mahamat Idriss Déby, walionyesha mnamo Januari 29, 2023 huko Ndjamena nia yao ya kuimarisha nguvu kwa pamoja kati ya Chad na Sudan. Kikosi kilichoundwa mwaka 2005 kufanya doria katika eneo lenye umbali wa kilomita 1,000 za mipaka ya pamoja ya nchi hizo mbili.

Rais wa Mpito wa Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan (kushoto) na Rais wa Chad Mahamat Idriss Déby.
Rais wa Mpito wa Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan (kushoto) na Rais wa Chad Mahamat Idriss Déby. © Photos AFP - Montage RFI
Matangazo ya kibiashara

Mnamo Januari 29, 2023, mkutano ulifanyika kati ya Sudan na Chad. Rais wa mpito wa Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, alikuwa Ndjamena, ambako alijadiliana na mwenzake Mahamat Idriss Déby. Waliungumzia masuala mbalimali hususan diplomasia, uchumi, na hasa usalama.

Viongozi hao wawili wa nchi walitangaza kwamba wanataka kuimarisha kikosi cha pamoja cha Chad na Sudan. Kikosi kilichoundwa mwaka 2005 kushika doria katika eneo lenye umbali wa kilomita 1,000 za mipaka ya kawaida na ambacho kinaonekana kimelegalega katika miaka ya hivi karibuni.

Wanasema wanataka kuimarisha mazungumzo, hasa katika suala la habari na kijasusi kati ya idara za usalama za nchi hizo mbili, pamoja na ushirikiano wa mahakama.

Matukio ya mpaka hutokea mara kwa mara

Nia hii ya kuongeza mazungumzo inakuja wakati ambapo matukio katika mipaka yao ya pamoja hutokea mara kwa mara.

Kama ukumbusho, miezi sita iliyopita, wizi wa ng'ombe ulibadilika na kuwa mapigano baina ya jamii, na kusababisha vifo vya watu thelathini.

Na kisha kuna wasiwasi mwingine kwa Ndjamena, anasisitiza mtafiti: habari za hivi karibuni zinaripoti uwepo wa makundi yenye silaha na hasa kundi jipya la waasi kusini mwa Chad, wakati huu kwenye mpaka na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Hatimaye Ndjamena pia ingependa kuamilisha tena ushirikiano wake wa usalama na Bangui.

Wakati huo huo , wakuu wa nchi hizi mbili waliamua kufanya kongamano la usalama na maendeleo kabla ya mwisho wa mwaka huko Abéché.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.