Pata taarifa kuu
USALAMA BARABARANI

Chad: Watu 20 wafariki baada ya basi na lori kugongana

Watu 20 wamefariki usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa katikati mwa Chad wakati basi lao lilipogonga lori lililoharibika likiwa katika mwendo wa kasi, wizara ya uchukuzi imesema.

Ajali mbaya zinazohusisha mabasi ambayo mara nyingi hujaa kupita kiasi na kusafiri kwa mwendo wa kasi hutokea mara kwa mara katika barabara za Chad.
Ajali mbaya zinazohusisha mabasi ambayo mara nyingi hujaa kupita kiasi na kusafiri kwa mwendo wa kasi hutokea mara kwa mara katika barabara za Chad. © Djimet Wiche/AFP
Matangazo ya kibiashara

Ajali hiyo, ambayo pia imesababisha watu saba kujeruhiwa, wakiwemo wawili wakiwa "katika hali mbaya", ilitokea takriban kilomita 500 mashariki mwa mji mkuu N'Djamena, katika eneo la jangwa kilomita 35 kutoka mji wa Oum-Hadjer, kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa wizara ya uchukuzi.

Basi hilo la shirika la usafiri huko N'Djamena lilikuwa limeondoka katika mji mkuu siku ya Alhamisi kuelekea mji wa Abéché, mji mkuu wa jimbo la Ouaddaï, "likiwa limebeba watu 31", kulingana na taarifa hiyo. Ajali hiyo ilitokea muda mfupi kabla ya saa sita usiku: basi hilo liligonga lori kubwa "lililoharibika na kuegeshwa barabarani".

"Kwa mujibu wa vielelezo vya kwanza vya uchunguzi, sababu zilizobainishwa ni kutofuata sheria za usalama barabarani inapotokea gari kuharibika, mwendo kasi kupita kiasi (…), uchovu na uzembe wa dereva" wa basi, imebini wizara ya uchukuzi.

Watu 18 walifariki papo hapo na wawili katika hospitali ya Abéché, jiji la tatu la nchi, ambapo majeruhi walisafirishwa.

Ajali mbaya zinazohusisha mabasi ambayo mara nyingi hujaa kupita kiasi na kusafiri kwa mwendo wa kasi hutokea mara kwa mara katika barabara za Chad. Mnamo Februari 28, 2022, watu 33 walifariki na 54 kujeruhiwa mabasi mawili kugongana, katikati ya usiku na kwenye barabara hiyo ya N'Djamena-Abéché, karibu na mji wa na Oum-Hadjer.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.