Pata taarifa kuu
CHAD-SIASA

Chad yakubali vyama vya upinzani viendelee na shughuli zake

Serikali ya Chad, imeondoa marufuku kwa vyama vya siasa vya upinzani kuendelea na shughuli zake, ikiwemo mikutano ya kisiasa.

Mahamat Idriss Deby Itno kiongozi wa Chad
Mahamat Idriss Deby Itno kiongozi wa Chad AFP - DENIS SASSOU GUEIPEUR
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya kupita kwa miezi kadhaa ya marufuku hayo, baada ya kutokea kwa maandamano ya wapinzaji jijini Ndjamena  na miji mingine, dhidi ya serikali  mwaka uliopita.

Maafisa wa usalama, walitumia nguvu kupita kiasi, kupambana na waandamanaji na hata kuwakamata baadhi ya wanasiasa wa upinzani, huku wengine wakitoroka, kitendo ambacho kilaaniwa na jumuiya ya Kimataifa.

Wanaharati wanasema mamia ya watu walipoteza maisha katika maandamano hayo, lakini serikali ilisema watu karibu 50 ndio waliouawa.

Waziri wa Mambo ya ndani Limane Mahamat, amesema wanasiasa wa upinzani sasa wanaweza kuendelea na shughuli zao ili mradi wafuate sheria za nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.