Pata taarifa kuu

Sudan na Israel zakubaliana 'kufufua uhusiano '

Sudan na Israel "zimekubaliana kuelekea kufufua uhusiano" wakati wa ziara ya kwanza rasmi ya mkuu wa diplomasia kutoka taifa la Israel mnamo Alhamisi, Februari 2. Haya ni kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan. 

Kiongozi wa utawala wa kijeshi nchini Sudan, Sudan Abdel Fattah al-Burhan, akifanya mkutano na waandishi wa habari Oktoba 26, 2021 mjini Khartoum siku moja baada ya mapinduzi yake.
Kiongozi wa utawala wa kijeshi nchini Sudan, Sudan Abdel Fattah al-Burhan, akifanya mkutano na waandishi wa habari Oktoba 26, 2021 mjini Khartoum siku moja baada ya mapinduzi yake. © ASHRAF SHAZLY/AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Mnamo Januari 2021, Khartoum ilitangaza kufuata Mkataba wa Abraham, ambapo mataifa mengine matatu ya Kiarabu yaliitambua Israel, na hivyo kupata usaidizi wa kifedha kutoka Marekani, baada ya kuondolewa kwenye orodha ya Marekani ya mataifa yanayotuhumiwa kufadhili ugaidi. 

Lakini tofauti na Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain na Morocco, Sudan hadi sasa imeshindwa kufuatilia makubaliano hayo kwa hatua madhubuti za kuimarisha uhusiano.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.