Pata taarifa kuu

Norway yasikitishwa na ushawishi wa Moscow na Beijing barani Afrika

Norway ina wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa vitimbi kwa nchi za Magharibi ambako Urusi na China zinachochea katika nchi zinazoendelea, hasa barani Afrika, waziri wake wa misaada ya maendeleo amesema Jumatatu.

ais wa China Xi Jinping, kulia, na Rais wa Urusi Vladimir Putin wakipiga picha kabla ya mazungumzo yao mjini Beijing, China, Feb. Tarehe 4, 2022. Mwaka mmoja baada ya vita vya Urusi dhidi ya Ukraine, China inatoa pendekezo la vipengele 12 ili kukomesha mapigano.
ais wa China Xi Jinping, kulia, na Rais wa Urusi Vladimir Putin wakipiga picha kabla ya mazungumzo yao mjini Beijing, China, Feb. Tarehe 4, 2022. Mwaka mmoja baada ya vita vya Urusi dhidi ya Ukraine, China inatoa pendekezo la vipengele 12 ili kukomesha mapigano. AP - Alexei Druzhinin
Matangazo ya kibiashara

"Ikiwa kitu kinanifanya nikose usingizi, ni jinsi hali ya kutoaminiana inavyoongezeka na jinsi baadhi ya nchi hivi leo zinavyochochea vitimbi hivi," Anne Beathe Tvinnereim almesema wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa kigeni.

"Sidhani kuwa ni sadfa kwamba (Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov) amefanya safari kadhaa barani Afrika na tunaona nia ya China katika Afrika," ameongeza.

"Huu ni mfano mmoja tu kati ya mingi (ambayo inaonyesha) kwa nini ni muhimu nchi kama Norway na wenzao wasijitoe badala yake tuongeze msaada wetu wa kimataifa kwa sababu nchi zinazoendelea zinahitaji kujua kwamba hazijasahaulika," alisema.

Pia amesisitiza haja ya msaada kwa Ukraine kutoficha majanga mengine na haja ya kuhakikisha usalama wa chakula mahali pengine duniani. Nchi maskini "hazikuchagua kuhusika katika utengano huu", alisema. "Nadhani ni kwa manufaa ya Norway na Magharibi kurudisha nyuma mgawanyiko huu kwa njia zote tulizo nazo, ikiwa ni pamoja na misaada ya maendeleo."

"Hatuwezi kuwa na hatari ya kufika katika hali ambayo nchi zinazoendelea zinahisi kuwa ni Magharibi dhidi ya nyingine," alisisitiza.

Kando na msaada mkubwa kwa Ukraine wa pesa za Norway bilioni 75 (euro bilioni 6.8) katika kipindi cha miaka mitano, Norway itatenga pesa zake zaidi ya bilioni 5 mwaka huu kwa nchi masikini ambazo zimeathiriwa na mzozo huo, haswa kutokana na kupanda kwa bei ya vyakula. .

Lakini serikali ya mrengo wa kati imekosolewa vikali kwa kuvunja, katika bajeti yake ya 2023, na utamaduni kwamba nchi tajiri ya Skandinavia inatoa 1% ya pato lake la kitaifa kwa misaada ya maendeleo.

Mwaka huu, Oslo inapaswa kutenga 0.97%. Tofauti ambayo Bi. Tvinnereim alihalalisha na kushuka kwa kiwango kikubwa kwa mapato ya kitaifa ya Norway, ambayo ilikuzwa ghafla na kuruka kwa bei ya hidrokaboni, ambayo nchi hiyo ni moja ya wazalishaji wakuu barani Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.