Pata taarifa kuu

Ghasia dhidi ya wahamiaji: Benki ya Dunia yasimamisha mpango wake nchini Tunisia

Benki ya Dunia (WB) itasitisha "hadi itakapotangazwa tena" mfumo wake wa ushirikiano na Tunisia, baada ya mashambulizi yaliyolenga wahamiaji nchini humo, kufuatia hotuba ya Rais wa Tunisia Kaïs Saïed mwishoni mwa mwezi Februari akilaani "makundi ya wahamiaji haramu".

Makao makuu ya Benki ya Dunia mjini Washington.
Makao makuu ya Benki ya Dunia mjini Washington. © AP/Andrew Harnik
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na barua iliyotumwa kwa timu zake na rais wa WB, David Malpass, ambayo AFP iliweza kupata kopi siku ya Jumatatu, benki hiyo haikuwa na uwezo wa kuendelea na misheni yake papo hapo "kutokana na hali hii", ili " usalama na ushirikishwaji wa wahamiaji na walio wachache ni sehemu ya maadili kuu ya ushirikishwaji, heshima na kupinga ubaguzi wa rangi" ya WB.

Uamuzi huo unahusu Mfumo wa Ubia wa Nchi (CPF kwa Kingereza), ambao unatumika kama msingi wa ufuatiliaji na Bodi ya Wakurugenzi (CA) ya WB ili kutathmini na kusaidia nchi katika programu zake za misaada. Kwa hakika, taasisi haiwezi tena kuzindua mpango mpya wa usaidizi na nchi hadi Bodi itakapokutana na imeamua kuahirisha mkutano huu wa Tunisia "hadi itakapoamuliwa tena", kulingana na barua ya Bw. Malpass.

"Miradi inayofadhiliwa itaendelea kufadhiliwa na miradi inayoendelea, itaendelea," kilisema chanzo kilicho karibu na WB. Hata hivyo, WB inaonya kuhusu uwezekano wa kupungua kwa hatua zake kwenye kutokana na utekelezaji wa hatua za usalama, hasa kwa wafanyakazi wake kutoka  Kusini mwa Jangwa la Sahara na familia zao.

"Tunisia ina utamaduni wa muda mrefu wa uwazi na uvumilivu jambo ambalo linahimizwa na watu wengi nchini," alisisitiza David Malpass katika barua yake kwa wafanyakazi wa WB. Iwapo hatua zinazochukuliwa na serikali ya Tunisia "kuwalinda na kusaidia wahamiaji na wakimbizi katika hali hii ngumu sana" zinakwenda "vizuri", WB inahakikisha kwamba "itatathmini kwa uangalifu na kufuatilia athari zake".

Rais wa Tunisia Kaïs Saïed alitangaza mnamo Februari 21 katika hotuba yake kwamba "hatua za haraka" zilikuwa muhimu "dhidi ya uhamiaji haramu wa raia kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara", akiongea hasa juu ya "makundi ya wahamiaji haramu" ambao kuwasili kwao ni jambo la kawaida. "biashara ya uhalifu iliyoanzishwa mwanzoni mwa karne hii ili kubadilisha muundo wa raia wa Tunisia".

Matamshi haya yalishutumiwa vikali na mashirika yasiyo ya kiserikali na wanaharakati wa haki za binadamu. Pia yamezua hali ya hofu miongoni mwa wahamiaji wa kusini mwa jangwa la Sahara ambao wameripoti kuongezeka kwa mashambulizi dhidi yao na wengi kukimbilia kwenye balozi zao ili kurejeshwa makwao.

Kwa mujibu wa takwimu rasmi zilizonukuliwa na Jukwaa la Haki za Kiuchumi na Kijamii la Tunisia (FTDES), Tunisia, ambayo ina wakazi milioni 12, ina wakazi zaidi ya 21,000 kutoka nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, wengi wao wakiwa hawana vibali vya kuishi nchini humo (wahamiaji haramu).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.