Pata taarifa kuu
SIASA-UCHAGUZI

Makamu wa Rais wa Afrika Kusini David Mabuza ajiuzulu

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amerasimisha siku ya Alhamisi kutoka Bungeni mjini Cape Town kuondoka kwa makamu wake wa rais David Mabuza, anayejiuzulu, huku mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri yakitarajiwa katika wiki zijazo.

Makamu wa Rais wa Afrika Kusini David Mabuza katika hafla ya huko Carnarvon, Afrika Kusini, Julai 13, 2018.
Makamu wa Rais wa Afrika Kusini David Mabuza katika hafla ya huko Carnarvon, Afrika Kusini, Julai 13, 2018. AFP/Mujahid Safodien
Matangazo ya kibiashara

Paul Mashatile, mwenye umri wa miaka 61, aliyechaguliwa mwezi Desemba kuwa naibu kiongozi wa chama cha ANC (African National Congress), chama cha kihistoria kilicho madarakani, anatarajia kuchukuwa nafasi yake.

David Mabuza, 62, "ameonyesha nia ya kujiuzulu kwenye wadhifa wake", ametangaza mkuu wa nchi, akimshukuru makamu wake kwa "uungwaji mkono wake usiyotetereka" katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Bw. Mabuza alisema mapema mwezi huu kwamba aliwasilisha ombi la kujiuzulu.

Paul Mashatile, mwenye umri wa miaka 61, aliyechaguliwa mwezi Desemba kuwa naibu kiongozi wa chama cha ANC (African National Congress), chama cha kihistoria kilicho madarakani, anatarajia kuchukuwa nafasi yake. David Mabuza, kiongozi mwenye utata anayeitwa "Paka", alichukuliwa kuwa karibu na Jacob Zuma, rais wa zamani na mpinzani wa kisiasa wa milele wa Cyril Ramaphosa.

Wapinzani wake siku za nyuma walimshutumu kwa kuongoza "jeshi" la kibinafsi lililohusika na vitisho vya kisiasa na mauaji alipokuwa mkuu wa jimbo la Mpumalanga (kaskazini mashariki).

Cyril Ramaphosa, 70, aliteuliwa tena kuwa rais wa ANC mwezi Desemba, na kumpa muhula wa pili madarakani iwapo chama hicho kitashinda uchaguzi mkuu wa 2024. Anatazamiwa kutangaza mabadiliko ya serikali baada ya kuwasilishwa kwa bajeti ya serikali ya mwaka wiki ijayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.