Pata taarifa kuu

Watu 20 wafariki katika ajali ya barabarani nchini Afrika Kusini

Watu 20 walifariki dunia na karibu 60 kujeruhiwa nchini Afrika Kusini baada ya basi moja kugongana na gari la kijeshi, idara ya usafiri ya jimbo la Limpopo, kaskazii mwa Afrika Kusini, imesema siku ya Jumanne.

Ajali hiyo ilitokea Jumatatu katika barabara ya kitaifa huko Limpopo, kwenye mpaka na Zimbabwe.
Ajali hiyo ilitokea Jumatatu katika barabara ya kitaifa huko Limpopo, kwenye mpaka na Zimbabwe. RFI
Matangazo ya kibiashara

"Watu 20 walifariki katika ajali wakati lori la kubebea pesa lilipopoteza mwelekeo na kugongana uso kwa uso na basi lililokuwa likitokea upande mingine," Idara ya Uchukuzi imesema katika taarifa.

Ajali hiyo ilitokea mwendo wa saa 3:00 mchana sawa na sa saba kamili siku ya Jumatatu kwenye barabara ya kitaifa huko Limpopo, jimbo lililo kaskazini mwa nchi, kwenye mpaka na Zimbabwe. Takriban watu 60 walijeruhiwa, 10 kati yao wako atika hali ya mahtuti. Walipelekwa hospitali.

Timu ya polisi ya kupiga mbizi kwa sasa inatafuta katika mto chini ya barabara kutafuta "watu ambao wanaweza kuwa walisombwa" na maji. Chanzo cha ajali hiyo mbaya bado hakijabainika, lakini "eneo hilo liliathiriwa na mvua kubwa," msemaji wa idara ya uchukuzi Tidimalo Chuene ameliambia shirika la habari la AFP.

Afrika Kusini imekumbwa na mvua kwa siku kadhaa ambazo zimesababisha mafuriko katika majimbo kadhaa. Takriban watu saba waliuawa, na wangine kadhaa hawajulikani walipo. Serikali imetangaza hali ya maafa ya kitaifa.

Afrika Kusini ina mojawapo ya mitandao ya barabara iliyoendelea zaidi barani humo lakini ni miongoni mwa nchi zinazofanya vibaya katika masuala ya usalama barabarani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.