Pata taarifa kuu

Ramaphosa atangaza 'janga la kitaifa' nchini Afrika Kusini kutokana na mgogoro wa umeme

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametangaza hali ya janga la kitaifa siku ya Alhamisi jioni katika jaribio la kukomesha tatizo kubwa la umeme ambalo linadhoofisha maisha na uchumi wa kila siku wa nchi hii iliyostawi kiviwanda barani Afrika.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa wakati kihutubia taifa mjini Cape Town Februari 9, 2023.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa wakati kihutubia taifa mjini Cape Town Februari 9, 2023. AP
Matangazo ya kibiashara

Kwa miezi kadhaa, Waafrika Kusini milioni 60 wamelazimika kupika, kufua nguo na kuchaji simu zao nyakati fulani za mchana pekee.

Kwa miezi kadhaa, Waafrika Kusini milioni 60 wamelazimika kupika, kufua nguo na kuchaji simu zao nyakati fulani za mchana. Nchi haina umeme na inautoa kwa mgao uliopangwa. Mgao huo mara nyingi hudumu hadi saa 12 kwa siku kadhaa, uhaba huo ukiwa mbaya zaidi tangu mwaka jana.

"Tunatangaza janga la kitaifa ili kukabiliana na tatizo la umeme na athari zake," mara moja, Bw Ramaphosa, 70, alisema kutoka makao makuu ya manispaa yaJiji la Cape Town ambako alitoa hotuba yake ya kila mwaka kuhusu hali mambo nchini Afrika Kusini.

"Katika hali ya kukipekee, hatua za kipekee huchukuliwa," aliongeza. "Kwa sasa, kazi kubwa ni kupunguza kwa kiasi kikubwa mgao unaoendelea na katika miezi ijayo ili kukomesha kuondokana kabisa na hali hiyo".

Chama tawala (ANC, African National Congress) kilisema wiki iliyopita kwamba kimetoa "maelekezo ya wazi" na kuitaka serikali kupitisha kifungu hiki.

Misaada kwa makampuni, hasa katika sekta ya chakula, hasa walioathirika na mgogoro, itatolewa, alitangaza Mkuu wa Nchi. Hospitali na mitambo ya kusafisha maji taka itaepushwa na mgao wa umeme. Waziri wa umeme anayehusishwa katika ofisi ya rais atateuliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.