Pata taarifa kuu

Wananchi wa Afrika Kusini wasubiri hotuba ya rais wao kuhusu tatizo la umeme

Raia milioni 60 wa Afrika Kusini ambao hawana umeme kwa miezi kadhaa na wale ambao wanapata huduma hiyo hadi karibu saa 12 kwa siku wanamngoja Rais Cyril Ramaphosa kuhusu mzozo wa nishati unaoikumba nchi hiyo, wakati wa hotuba yake ya kila mwaka kuhusu ya hali ya nchi siku ya Alhamisi.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa wakati wa hotuba yake kwa wabunge Februari 10, 2022 katika Ukumbi wa Jiji la Cape Town.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa wakati wa hotuba yake kwa wabunge Februari 10, 2022 katika Ukumbi wa Jiji la Cape Town. © AP/Nic Bothma
Matangazo ya kibiashara

Sherehe kawaida hufanywa kwa shauku kubwa katika Bunge. Lakini jengo la kihistoria mjini Cape Town ambalo kwa kiasi fulani liliharibiwa na kisa cha uchomaji moto mwaka jana, rais atazungumza jioni kutoka katika Ukumbi wa Jiji la Cape Town..

Afrika Kusini imeendelea kukumbwa na mdororo wa kiuchumi na kijamii.

Nchi hii ambayo imekumbwa na mojawapo ya viwango vya juu zaidi vya ukosefu wa ajira duniani (32.9%), utabiri wa ukuaji wa Pato la Taifa kwa mwaka karibu sifuri (0.3%) na familia zilizokandamizwa na kupanda kwa bei za bidhaa, hasira juu ya uhaba wa umeme imesababisha maelfu ya watu kiingia mitaani. Katika wiki za hivi karibuni, maandamano yamezuka katika miji kadhaa ikiwa ni pamoja na Johannesburg, kwa wito wa upinzani na vyama vya wafanyakazi.

Uongozi mbaya na ufisadi

Tangu mwaka jana, mzozo wa nishati umeongezeka katika nchi hii iliyostawi kiviwanda barani Afrika, ikibaki nyuma katika mpito wa nishati safi. Kampuni ya umma ya Eskom, iliyolemewa na miaka mingi ya usimamizi mbovu na ufisadi uliokithiri chini ya utawala wa rais Jacob Zuma (2009-2018), haiwezi kuzalisha umeme wa kutosha katika vituo vyake vya zamani vya nishati ya makaa ya mawe ambavyo vinaathiriwa mara kwa mara na kuharibika.

Dawa pekee kwa sasa, kmgao wa umeme umepangwa mara kadhaa kwa siku, na kulazimisha nchi nzima kupika, kufua nguo na kuchaji simu kwa nyakati fulani pekee. Makampuni yanapoteza mamia ya mamilioni ya dola kila siku, kulingana na chama cha kikuu cha upinzani (DA, Democratic Alliance), ambacho kinakashifu uzembe wa serikali katika kutatua mgogoro huo.

Chama tawala cha African National Congress (ANC) kilitangaza wiki iliyopita kuwa kimetoa "maagizo ya wazi" na kuitaka serikali kutangaza hali ya maafa ili kupata fedha. Lakini kulingana na Dieter von Fintel, mwanauchumi katika Chuo Kikuu cha Stellenbosch, hatua hii ya "ishara" tu ingekuwa na nguvu ya kutuliza maoni ambayo tayari yamepoteza uaminifu, wakati shida halisi inayobaki katika ukweli kwamba "mgogoro wa mzunguko mfupi wa nishati utazima jaribio lolote la kufufua uchumi na sasa unawakilisha tishio kwa utulivu wa kijamii.

Chama chenye siasa kali za mrengo wa kushoto, EFF (Wapigania Uhuru wa Kiuchumi), kimeahidi kuvuruga hotuba ya rais. Akiwa amekumbwa na kashfa chafu ya fedha, Cyril Ramaphosa aliepuka kuondolewa madarakani mwezi Desemba, akiungwa mkono na ANC. Uchunguzi wa polisi bado unaendelea.

Chama hicho cha kihistoria kilimchagua tena kama kiongozi wake, kikihakikisha rais huyo mwenye umri wa miaka 70, ambaye bado ni maarufu na ambaye anaendelea kuwa mtu muhimu na bora, kwa muhula wa pili endapo ANC itashinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2024.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.