Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI - UMEME

Maandamano Afrika Kusini kulalamikia ongezeko la kukatika kwa umeme

Nchini Afrika Kusini, wafuasi wa chama cha Democratic Alliance (DA), wameandamana jijini Johannesburg, kulalamikia ongezeko la kukatika kwa umeme mara kwa mara nchini humo.

Raia nchini Afrika kusini wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kukatika kwa umeme kila mara
Raia nchini Afrika kusini wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kukatika kwa umeme kila mara © Siphiwe Sibeko / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji walikwenda katika makao makuu ya chama tawala ANC, wakiwa na mabango yaliyosomeka, imetosha.

John Steenhuisen ni kiongozi wa DA.

“Maandamano ya leo ni mwanzo wa kurejesha nguvu kwa raia wa Afrika Kusini ambao ndiyo wenye nguvu.”amesema John Steenhuisen.

Afrika kusini kwa muda sasa imekuwa inakabiliwa na changamoto za kukatika kwa umeme, raia wakieleza kushindwa kuendelea na biashara zao za kila siku.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.