Pata taarifa kuu

Maiti yatoweka kwenye jeneza kaburini nchini Afrika Kusini

Marehemu alivutwa kutoka chini ya jeneza alimokuwa amelazwa: Polisi wa Afrika Kusini imesema Jumatano kwamba imefungua uchunguzi "usiokuwa wa kawaida" baada ya wizi wa ajabu wa maiti katika makaburi.

Polisi pia imeitaka jamii ya Thembi Hadebe, kutulia baada ya tukio hilo na sio kutafuta “kulipiza kisasi”. Hakuna aliyekamatwa kufikia sasa.
Polisi pia imeitaka jamii ya Thembi Hadebe, kutulia baada ya tukio hilo na sio kutafuta “kulipiza kisasi”. Hakuna aliyekamatwa kufikia sasa. AFP
Matangazo ya kibiashara

"Mshukiwa au washukiwa walikata jeneza upande wa mguu na kuutoa mwili wa marehemu," Motlafela Mojapelo, msemaji wa polisi wa jimbo la kaskazini la Limpopo, ameliambia shirika la habari la AFP.

Siku ya Jumapili, ndugu wa Modike Masedi, aliyefariki mwaka mmoja uliopita akiwa na umri wa miaka 83, alienda kwenye makaburi ya kijiji hicho kuandaa kaburi kabla ya sherehe ya kuwakutanisha familia na jamaa.

Ndugu huyu ndipo aligundua kuwa kaburi lililojengwa kwa matofali ikifunikwa na jiwe nyeusi limefunguliwa. Shimo lilichimbwa pembeni, na mwili umetoweka.

Mkuu wa polisi wa eneo hilo Thembi Hadebe, ambaye amesema "ameshtuka", amesema katika taarifa yake kwamba ameamuru wahalifu au wizi hao wa makaburini "kufuatiliwa na kufikishwa mahakamani". Polisi pia imeitaka jamii ya Thembi Hadebe, kutulia baada ya tukio hilo na sio kutafuta “kulipiza kisasi”. Hakuna aliyekamatwa kufikia sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.