Pata taarifa kuu

Marekani na Afrika Kusini zataka kuimarisha ushirikiano wao dhidi ya ujangili

Afrika Kusini na Marekani zitaunda kitengo cha pamoja cha kufuatilia mtiririko wa fedha unaotokana na ujangili wa wanyama pori, ametangaza Jumatano Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen, akizuru nchi hii.

Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen.
Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen. © AP
Matangazo ya kibiashara

"Ili kulinda wanyamapori dhidi ya uwindaji haramu na kuvuruga biashara haramu inayotokana nayo, tunahitaji kufuata pesa kama vile tunavyofanya kwa uhalifu mwingine mbaya," Bi Yellen ameomba wakati wa ziara yake katika hifadhi ya wanyama kaskazini mwa mji mkuu Pretoria.

"Hii ni pamoja na kutambua na kukamata faida inayotokana na usafirishaji haramu wa wanyamapori," amesema. Kitengo husika kitaboresha upashanaji wa taarifa kati ya idara za kijasusi za kifedha ili kusaidia vyema huduma za polisi za nchi hizo mbili, ameongeza waziri wa Marekani.

Afrika Kusini ina karibu 80% ya vifaru duniani. Hii inafanya kuwa mahali pa ujangili kwa mnyama huyu ambaye yuko hatarini kutoweka, ikichochewa na mahitaji kutoka Asia, ambapo pembe za pachyderm, ambazo hutengenezwa kwa keratini, hutumiwa katika dawa za jadi.

Kulingana na shirika lisilo la kiserikali la Save the Rhino International, mwaka 2013 karibu faru 10,000 walitembea Hifadhi ya Kruger, hifadhi kubwa zaidi ya wanyama nchini Afrika Kusini, ikilinganishwa na zaidi ya 2,400 hivi sasa, kushuka kwa 75% katika chini ya miaka kumi. Ujangili nchini Afrika Kusini pia unalenga Pangolin na tembo.

Bi Yellen yuko katika ziara barani Afrika, mojawapo ya ziara za kwanza katika mfululizo wa ziara zinazotarajiwa za maafisa wakuu wa utawala wa Marekani tangu mwezi Desemba kuzinduliwa kwa mashambulizi ya kidiplomasia katika bara ambalo ni msingi wa ushindani mkali wa mahusiano ya kiuchumi na kisiasa kati ya mataifa makubwa , hasa China na Urusi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov alimtangulia Jumatatu kwenda Afrika Kusini, ambayo hivi karibuni ilitangaza luteka ya pamoja ya kijeshi mwezi Februari pamoja na majeshi ya majini ya Urusi na China kwenye pwani yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.