Pata taarifa kuu

Mvua nchini Afrika Kusini: Serikali yatangaza janga la kitaifa

Serikali ya Afrika Kusini imeamua kutangaza hali ya maafa ya kitaifa kwa kutarajia mvua zinazoendelea kunyesha nchini humo katika siku zijazo.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa wakati akitangaza janga la kitaifa mjini Cape Town Februari 9, 2023.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa wakati akitangaza janga la kitaifa mjini Cape Town Februari 9, 2023. AP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari, hatua hii inapaswa kufanya iwezekanavyo kuwezesha "majibu makubwa na ya uratibu", wakati mvua tayari zimesababisha uharibifu wa nyenzo katika mikoa tofauti pamoja na waathirika kadhaa. 

Kwa sasa nchi inajikuta katika mtego wa majanga mawili ya kitaifa kwa wakati mmoja kwani hatua hiyo pia imetumika tangu wiki iliyopita kuwezesha majibu ya shida ya umeme.

Hivi karibuni Rais Cyril Ramaphosa ambaye anakabiliwa na lawama na ghadhabu za wananchi, alitangaza "hali ya maafa nchini humo kufautia kukosekana huduma ya umeme na kuahidi kumaliza shida ya upungufu wa nishati ambayo inatishia utulivu wa kiuchumi na kisiasa nchini humo.

Kukatika kwa umeme kumekuwa sehemu ya maisha nchini Afrika Kusini kwa karibu miaka 16 sasa, lakini miezi kadhaa iliyopita nchi hiyo imekumbwa na tatizo kubwa la kusalia gizani bila ya huduma ya umeme.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.