Pata taarifa kuu

Kumi na mbili wafariki kutokana na mafuriko nchini Afrika Kusini

Takriban watu 12 wamefariki katika mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa nchini Afrika Kusini, ambapo hali ya maafa ya kitaifa imetangazwa, kuongezeka kwa maji kunaathiri hasa mbuga ya watalii ya Kruger, kulingana na mamlaka. Ripoti iliyotangulia siku moja kabla iliripoti kuwa watu 7 walifariki.

Afisa wa huduma ya uokoaji ya polisi akiwatafuta watu waliopotea kwenye vifusi kufuatia mafuriko nje ya Durban Aprili 15, 2022.
Afisa wa huduma ya uokoaji ya polisi akiwatafuta watu waliopotea kwenye vifusi kufuatia mafuriko nje ya Durban Aprili 15, 2022. AFP - PHILL MAGAKOE
Matangazo ya kibiashara

Hali mbaya ya hewa imesaabisha waathiriwa katika majimbo manne - kati ya tisa kwa jumla - kwenye ukingo wa mashariki mwa nchi, ambayo sehemu kubwa yanagusa Bahari ya Hindi, msemaji wa wizara Lungi Mtshali ameliambia shirika la habari la AFP. "Jimbo la Mpumalanga (kaskazini mashariki) linaonekana kuathirika zaidi hadi sasa. Hali katika Hifadhi ya Kruger kwa kweli si nzuri," amesema.

Hifadhi kubwa zaidi ya kitaifa nchini, ambayo ina ukubwa wa hekta milioni 2, inapitiwa na mito kadhaa, ambayo mingi imekuwa na mafuriko tangu wikendi iliyopita, kulingana na Taasisi ya Kitaifa ya Utabiri wa Hali ya Hewa (SAWS).

"Kutembelea mbuga hiyo kumezuiliwa kwa sababu baadhi ya barabara zimeharibika. Lakini hali bado inadhibitiwa," Isaac Phaahla, msemaji wa shirika la hifadhi za taifa (SanPark), ameliambia shirika la habari la AFP. Kambi kadhaa ndani ya hifadhi hiyo zilihamishwa kutokana na hali iliyokuwa ikiripotiwa siku zilizopita.

Mvua zilianza kunyesha nchini wiki iliyopita, zikisababishwa na baridi kali ya ghafla katikati ya msimu wa joto. Zaidi ya milimita 200 za mvua zilinyesha kwa siku moja katika baadhi ya maeneo, mtabiri wa SAWS Puseletso Mofokeng ameliambia shirika la habari la AFP.

Mvua zaidi zinatarajiwa katika kipindi chote cha wiki kukiwa na hali mbaya ya joto wakati huu, Mofokeng alionya, akiongeza kuwa "maji ni mengi, maji hayawezi kufyonzwa na udongo na mafuriko kutokea kwa urahisi zaidi".

Ofisi ya rais ilitangaza hali ya maafa ya kitaifa siku ya Jumatatu. Serikali inapanga kutoa "makazi ya muda, chakula na mablanketi kwa watu ambao wamepoteza makazi yao, pamoja na ukarabati wa gharama kubwa wa miundombinu". Uharibifu mkubwa tayari umeripotiwa huku barabara na madaraja kuharibiwa pamoja na hospitali kuathirika.

Nchi hiyo ilikumbwa na mafuriko mabaya zaidi mwaka jana katika historia yake kukumba mji wa pwani wa Durban (kusini mashariki). Mvua kubwa ilisababisha maporomoko ya matope makubwa yaliyosomba kila kitu. Hali hii mbaya ya hewa ilisababisha vifo vya zaidi ya watu 400 na wengi kukosekana, huku uharibifu ukiwa ni makumi ya mamilioni ya euro.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.