Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Gemfields yasitisha shughuli zake Msumbiji baada ya mashambulizi ya wanajihadi

Kampuni ya uchimbaji madini ya Uingereza ya Gemfields ilitangaza siku ya Jumanne kwamba imesitisha shughuli za uchunguzi kaskazini-mashariki mwa Msumbiji, eneo linalokumbwa na ghasia za wanajihadi kwa zaidi ya miaka mitano, kufuatia shambulio kilomita chache kutoka kwa moja ya maeneo inakoendesha shughuli zake.

Zaidi ya wanajeshi 3,000 wa Kiafrika walitumwa mara moja kusaidia jeshi la Msumbiji. Mashambulizi yamepungua kwa kasi lakini mashambulizi ya hapa na pale yanaendelea.
Zaidi ya wanajeshi 3,000 wa Kiafrika walitumwa mara moja kusaidia jeshi la Msumbiji. Mashambulizi yamepungua kwa kasi lakini mashambulizi ya hapa na pale yanaendelea. AP - Marc Hoogsteyns
Matangazo ya kibiashara

Kampuni ya Gemfields inachimba madini ya ruby (mfalme wa madini) huko Cabo Delgado, jimbo maskini la Msumbiji lenye Waislamu wengi, kwenye mpaka na Tanzania. Mgodi wake wa Montepuez, takriban kilomita 200 magharibi mwa mji mkuu wa mkoa Pemba na ambao shughuli zake hazijaathiriwa, ni moja ya hifadhi kubwa zaidi za mawe hayo ya thamani duniani.

Usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu, shambulio lililenga kijiji cha Nairoto, kama kilomita kumi na tano kutoka eneo la uchunguzi la Gemfields, kampuni ya madini ilisema katika taarifa, bila kutaja majeruhi yoyote. "Mchakato wa kuwahamisha wafanyakazi na watoa huduma umezinduliwa na shughuli kwenye eneo hilo zimekoma," kampuni hiyo imebainisha, ikiongeza kuwa inaendelea kuwasiliana na mamlaka ya Msumbiji.

Mwaka jana, shambulio katika mgodi karibu na eneo lake kuu huko Montepuez lililazimisha kampuni hii kusimamisha shughuli zake kwa muda. Mashambulizi ya makundi yenye silaha katika eneo hilo lenye utajiri wa gesi asilia yameua zaidi ya watu 4,500, wakiwemo zaidi ya raia 2,000, kulingana na shirika lisilo la kiserikali la Acled. Pia watu milioni moja walilazimika kuyatoroka makaazi yao, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Mnamo mwezi Machi- na Aprili 2021, shambulio kubwa katika jiji la bandari la Palma lililazimisha kampuni ya TotalEnergies kusimamisha shughuli zote kwenye eneo lake la baadaye la uchimbaji wa gesi asilia. Zaidi ya wanajeshi 3,000 wa Kiafrika walitumwa mara moja kusaidia jeshi la Msumbiji. Mashambulizi yamepungua kwa kasi lakini mashambulizi ya hapa na pale yanaendelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.