Pata taarifa kuu

Mwanajihadi ahukumiwa kifo, wengine kumi na moja kifungo cha maisha nchini Misri

Mahakama ya Misri imemhukumu mwanajihadi mmoja adhabu ya kifo na wengine 11 kifungo cha maisha baada ya kuwatia hatiani kwa kujiunga na "kundi la kigaidi" lenye uhusiano na kundi la Islamic State, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti siku ya Jumatano.

Tangu aingie madarakani mwaka 2014, Rais al-Sisi ameongoza ukandamizaji mkali dhidi ya Waislamu na wapinzani.
Tangu aingie madarakani mwaka 2014, Rais al-Sisi ameongoza ukandamizaji mkali dhidi ya Waislamu na wapinzani. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya Kupambana na Ugaidi ya Cairo pia imewahukumu washtakiwa wengine watatu kifungo cha miaka 15 jela na wengine mitatu hadi miaka 10 jela kwa "kuongoza na kujiunga na kundi la kigaidi kati ya mwaka 2015 na Septemba 7, 2019", gazeti la serikali la Al Ahram limeripoti, bila kufichua jina la kundi hilo. Watu wanne wameachiliwa kwa mujibu wa chanzo hicho. Hukumu hizo, zilizotolewa Jumanne, washtakiwa wanaweza kukata rufaa.

Baada ya jeshi kumuondoa madarakani rais wa Kiislamu Mohamed Morsi Julai 3, 2013, wakati huu likiongozwa na Marshal Sissi, ambaye baadaye alikuja kuwa Rais, Misri ilikumbwa na mfululizo wa mashambulizi yaliyofanywa na wanajihadi na Waislamu. Makumi ya maafisa na wanachama wa vikosi vya usalama waliuawa katika mashambulizi haya.

Tangu aingie madarakani mwaka 2014, Rais Abdel Fattah el-Sisi ameongoza ukandamizaji mkubwa dhidi ya waislamu na wapinzani, jambo ambalo limepelekea maelfu ya watu kufungwa jela.

Mahakama za Misri mara kwa mara hutoa hukumu za kifo au kifungo cha muda mrefu gerezani baada ya kesi nyingi, na hivyo kukosolewa na Umoja wa Mataifa na mashirika ya haki za binadamu. Mwaka jana, washtakiwa 215 walihukumiwa vifungo vya kuanzia miaka 10 jela hadi hukumu ya kifo katika uamuzi mmoja.

Kulingana na shirika moja la haki za Binadamu nchini Misri, "washtakiwa 39 walihukumiwa kifo" mnamo mwezi Januari 2023, na wengine 46 walipata "hukumu za (kifo) za muda" wakisubiri idhini ya Mufti Mkuu, utaratibu rasmi katika kesi za hukumu ya kifo. Misri ilitekeleza idadi kubwa ya tatu ya watu walionyongwa duniani mwaka 2021, baada ya China na Iran, kulingana na shirika la kimataifa la haki za binadamu la Amnesty International.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.