Pata taarifa kuu

CHAN 2023: Timu ya Morocco haikuondoka kuelekea Algeria

Baada ya saa tatu kwenye chumba cha mapumziko cha watu mashuhuri cha uwanja wa ndege wa Rabat-Salé, siku ya Ijumaa Januari 13, wachezaji wa Morocco wameamua kurejea nyumbani kutokana na kukosa kibali cha kuondoka kutoka mamlaka ya Algeria. 

Wachezaji wa timu ya soka ya Morocco wakiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Rabat Januari 13, 2023.
Wachezaji wa timu ya soka ya Morocco wakiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Rabat Januari 13, 2023. AFP - FADEL SENNA
Matangazo ya kibiashara

Timu ya taifa ya Morocco, ambayo ingelishiriki michuano ya soka ya Mataifa ya Afrika (CHAN), ilikuwa Ijumaa Januari 13 asubuhi kwenye uwanja wa ndege wa Rabat-Salé wakisubiri kwenda Algeria. Ndege ya Royal Air Maroc (RAM) ilikuwa ikisubiri ruhusa kutoka mamlaka ya Algeria.

Timu ya Morocco yaondoka kwenye uwanja wa ndege kwa kukosa kibali

Simba wa Atlas walikuwa wakisubiri kibali kutoka Algiers kwa ajili ya kuondoka kwenda kushiriki michuano ya CHAN. 

"Wachezaji wamekuwa wakijiandaa kwa miezi kadhaa, tumeweka kila kitu ili kuwaandaa vizuri iwezekanavyo, lakini kwa kukosekana kwa majibu mazuri kutoka mamlaka ya Algeria, hatutaweza kucheza CHAN. Vijana hawa walitaka kushiriki katika michuano hiyo na kuonyesha, pia, kiwango chao cha kucheza wakiwa na nia ya kushinda michuano hiyo kama ile ya miaka iliyopita,” ametangaza Fouzi Lekjaa, rais wa shirikisho la Soka la Morocco, FRMF, wakati wachezaji walipokuwa wakitoka kwenye uwanja wa ndege.

Alhamisi jioni, Wizara ya Mambo ya Nje ya Morocco ilitangaza kwamba timu ya Morocco itashiriki CHAN nchini Algeria licha ya taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa mapema siku hiyo kwenye tovuti ya Shirikisho la Soka la Morocco.

Michuano hii, iliyotengwa kwa ajili ya wachezaji wanaoshiriki michuano ya kitaifa, itafanyika kuanzia Januari 13 hadi Februari 4 nchini Algeria.

Algiers ilifunga anga yake mnamo Septemba 22, 2021 kwa ndege zote za kiraia na za kijeshi za Morocco baada ya kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na Rabat. Mgogoro huu mkubwa unachochewa na suala tete la Sahara Magharibi, katika muktadha wa mivutano ya kudumu kati ya majirani hao wawili maadui.

Atlas Lions - moja ya vigogo wa soka barani Afrika - wameshinda CHAN mara mbili, mwaka wa 2021 na 2018.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.