Pata taarifa kuu

Sahara Magharibi: Algeria yasitisha mkataba wa ushirikiano na Uhispania

Tangazo hilo lilitolewa Jumatano Juni 8 na taarifa ya ofisi ya rais wa Algeria. Ni hatua iliyochukuliwa "haraka" kufuatia Madrid kugeuza faili la Sahara Magharibi.

Mtu huyu akishikilia bendera ya vuguvugu la Polisario mnamo Februari 3, 2017 katika eneo la Al-Mahbes.
Mtu huyu akishikilia bendera ya vuguvugu la Polisario mnamo Februari 3, 2017 katika eneo la Al-Mahbes. AFP
Matangazo ya kibiashara

Mnamo Machi 18, Uhispania, ambayo ilikuwa na nia ya kumaliza mzozo na Rabat, ilijiunga kwa mara ya kwanza tangu 1974 kwa msimamo wa Morocco. Msimamo ambao umeikasirisha Algeria, mshirika mkuu wa vuguvugu linalodai uhuru la Saharoui, Polisario Front.

Tangu Uhispania ilipotoka katika msimamo wa kutoegemea upande wowote ambao ilikuwa ikiutetea kila mara kuhusu hati ya Sahrawi, Algeria haijaacha kuonyesha kuudhika kwake. Baada ya kutishia kurekebisha bei ya gesi iliyouzwa kwa Uhispania, kwa sasa imesitisha mkataba wa urafiki, ujirani mwema na ushirikiano uliofikiwa mnamo mwaka 2002.

Mkataba kufiki sasa ulikuwa ukijikitakwenye mazungumzo ya kisiasa, lakini pia maendeleo ya ushirikiano katika nyanja za kiuchumi, fedha, elimu na ulinzi.

Ofisi ya rais imehalalisha uamuzi huu wa kusimamishwa kwa mkataba huo ikibaini kwamba nafasi mpya ya mamlaka ya Uhispania ni "ukiukaji wa majukumu yake ya kisheria, maadili na kisiasa" na inashutumu uungaji mkono wa Uhispania kwa hati haramu na isiyo halali ya uhuru wa ndani.

Uhispania, kwa upande wake, inasikitishwa na uamuzi wa Algeria. inasema "inaichukulia Algeria kuwa nchi jirani na rafiki" na ainataka kuendelea kuendeleza uhusiano wa ushirikiano na Algiers.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.