Pata taarifa kuu

Soka: Morocco yafuta ushiriki wake katika CHAN nchini Algeria

Morocco imetangaza Alhamisi kufuta ushiriki wake katika Michuano ya Mataifa ya Afrika (CHAN), mashindano ya wachezaji wa ndani, kutokana na hatua ya Algeria kuzifungia ndege za Morocco kufanya safari nchini humo, kutokana na hali ya mzozo kati ya majirani hao wawili wa Maghreb.

Simba wa Atlas ndio mabingwa mara mbili wa michuano ya Mataifa ya Afrika.
Simba wa Atlas ndio mabingwa mara mbili wa michuano ya Mataifa ya Afrika. REUTERS - CARL RECINE
Matangazo ya kibiashara

"Timu ya taifa ya sika ya Morocco haiwezi kusafiri kwenda Constantine nchini Algeria kwa vile idhini ya mwisho ya ndege yake ya Royal Air Maroc (RAM), ndege inayosafirisha rasmi timu za taifa za Morocco, kutoka Rabat kwenda Constantine haijathibitishwa," Shirikisho la Soka nchini Morocco (FRMF) limesema katika taarifa.

Hata hivyo Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), mratibu wa michuano ya CHAN, aliifahamisha FRMF mnamo Desemba 22 kwamba "idhini ya kimsingi imepatikana", kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari.

Michuano hii, iliyotengwa kwa ajili ya wachezaji wanaoshiriki michuano ya kitaifa, itafanyika kuanzia Januari 13 hadi Februari 4 nchini Algeria.

Saa 24 kabla ya kuanza, Shirikisho la Morocco "linatambua kwa masikitiko kwamba kupata kibali cha mwisho cha ndege ya RAM kutoka Rabat kwenda Constantine kwa bahati mbaya bado haijathibitishwa na CAF", imesisitiza FRMF.

Algiers ilifunga anga yake mnamo Septemba 22, 2021 kwa ndege zote za kiraia na za kijeshi za Morocco baada ya kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na Rabat. Mgogoro huu mkubwa unachochewa na suala tete la Sahara Magharibi, katika muktadha wa mivutano ya kudumu kati ya majirani hao wawili maadui.

Atlas Lions - moja ya vigogo wa soka barani Afrika - wameshinda CHAN mara mbili, mwaka wa 2021 na 2018.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.