Pata taarifa kuu

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu Sahara Magharibi akutana na kiongozi wa Polisario Front

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika Sahara Magharibi alimaliza ziara ya siku mbili katika kambi za wakimbizi huko Tindouf, Algeria siku ya Jumapili. 

Staffan de Mistura (kushoto) alikutana Jumapili na kiongozi wa Polisario Front, Brahim Ghali (kulia).
Staffan de Mistura (kushoto) alikutana Jumapili na kiongozi wa Polisario Front, Brahim Ghali (kulia). AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Baada ya ile ya mwezi Januari, hii ni ziara ya pili ya Staffan de Mistura katika eneo hilo tangu alipoteuliwa mwezi Novemba. Pia alitembelea Morocco mwezi Julai. Katika ziara yake ya Jumamosi na Jumapili: mikutano na wawakilishi wa Polisario Front, vuguvugu la wanaharakati linalopigania uhuru ambalo linatoa wito wa kura ya maoni ya kujitawala kwa Sahara Magharibi.

Staffan de Mistura alikutana kwa mazungumzo na kiongozi wa Polisario Front, Brahim Ghali,  siku ya Jumapili baada ya kukutana na wawakilishi wengine wa vuguvugu linalopigania uhuru siku moja kabla. Mkutano wa faragha, kulingana na shirika la habari nchini Algeria la APS, hasa kuandaa ripoti ambayo itawasilishwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika wiki zijazo.

Kabla ya ziara hii, msemaji wa Umoja wa Mataifa alibaini kwamba Staffan de Mistura " alikuwa akitarajia kuimarisha mashauriano na pande zote zinazohusika kuhusu matarajio ya kuendeleza mchakato wa kisiasa katika Sahara Magharibi".

Eneo ambalo Umoja wa Mataifa unalichukulia kama "lisilo la uhuru", na ambalo vuguvugu la Polisario Front, likiungwa mkono na Algeria, limekuwa limekuwa likipigana kwa miongo kadhaa dhidi ya vikosi vya Morocco, likitaka kura ya maoni ya kujitawala, wakati Morocco, ikipendekeza mpango huo wa kujitawala chini ya mamlaka yake.

Siku ya Jumapili jioni, Oubi Bouchraya, mjumbe wa uongozi wa Polisario Front katika ukanda wa Ulaya na Umoja wa Ulaya, alithibitisha kwamba chama chao kimejitolea kuwezesha kazi ya mjumbe wa Umoja wa Mataifa, huku akiendelea kutetea haki ya kujitawala kwa eneo hilo.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Sahara Magharibi anatazamiwa kuendelea na ziara yake mjini Algiers leo, kisha kuelekea Nouakchott, Mauritania, Jumamosi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.