Vita vyapamba moto katika Sahara Magharibi, pande katika mzozo zashtumiana
Kwa mwaka mmoja sasa, wapiganaji wanaotaka kujitenga wa Saharawi kutoka kundi la Polisario wameanza tena operesheni zao za kijeshi dhidi ya jeshi la Morocco, baada ya takriban miongo mitatu ya kusitisha mapigano.
Imechapishwa:
Mgogoro usio na ulinganifu ambao wanatumaini utaanzisha tena mazungumzo kuhusiana na eneo hili lenye hadhi linayogombaniwa, katikati ya mvutano wa kidiplomasia kati ya Morocco na Algeria.
Hivi karibuni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliashiria kuanza tena mapigano kati ya Morocco na Harakati ya Ukombozi wa Sahara Magharibi ya Polisario katika eneo hilo linalozozaniwa na kutangaza kuwa, hali ya mambo katika eneo hilo mwaka mmoja uliopita imekuwa mbaya kwa kiasi kikubwa.
Morocco inalitambua eneo la Sahara Magharibi kuwa sehemu ya ardhi yake; hata hivyo Harakati ya Polisario ambayo kimataifa inatambuliwa kama mwakilishi wa wananchi wa eneo la Sahara Magharibi, imekuwa ikipigania uhuru wa eneo hilo kwa miaka mingi sasa.
Vita vya kupigania uhuru baina ya harakati ya Polisario na Morocco vilianza mwaka 1975 na kuendelea hadi mwaka 1991 na kisha pande mbili zilisitisha mapigano kwa upatanishi wa Umoja wa Mataifa.
Katika ripoti yake ya hivi karibuni mbele ya Baraza la Usalama, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alisema kuwa, Harakati ya Polisario mwezi Novemba mwaka jana baada ya vuta nikuvite na Morocco ilitangaza kuwa haitaheshimu tena mapatano hayo ya usitishaji vita kati yake na Morocco.