Pata taarifa kuu
MOROCCO-USHIRIKIANO

Sahara Magharibi: Mahakama ya Ulaya yavunja mikataba miwili ya kibiashara na Morocco

Mahakama ya Umoja wa Ulaya imebatilisha mikataba miwili ya kibiashara kati ya Morocco na Umoja wa Ulaya. Kuvunjwa huku kwa mikataba hiyo kunakuja kufuatia rufaa ya wanaharakati wanaotaka kujitenga kwa jimbo lao kutoka kundi la  Polisario Front.

Nembo ya mahakama ya Umoja wa Ulaya, huko Luxembourg, Januari 13, 2021.
Nembo ya mahakama ya Umoja wa Ulaya, huko Luxembourg, Januari 13, 2021. AFP - JOHN THYS
Matangazo ya kibiashara

Mnamo mwaka 2019, mikataba miwili ya kibiashara kati ya Morocco na Umoja wa Ulaya ilianza kutekelezwa. Mkataba wa kwanza ni wa kilimo na unahusu matumizi ya ushuru kwa bidhaa kutoka Sahara Magharibi. Wa pili ni mkataba wa uvuvi ambao unaruhusu meli kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kutumia maji ya bahari ya Atlantiki, ikiwa ni pamoja na yale yaliyo karibu na Sahara Magharibi.

Jumatano hii, mahakama ya Umoja wa Ulaya imebatilisha maikataba hii. Hukumu ya mahakama ya mwanzo ambayo inatoa nafasi ya miezi miwili kwa utawala wa kifalme nchini Morocco kukata rufaa juu ya uamuzi huu. Wakati huo huo, biashara kati ya Morocco na Umoja wa Ulaya itaendelea. Na ikiwa suala hili linaonekana ni la kisheria, lakini kwa kweli ni la kisiasa.

Kundi la Polisario Front likaribisha uamuzi  wa Mahakama ya umoja wa Ulaya

Mikataba iliyofikiwa kati ya Umoja wa Ulaya na Morocco ilisainiwa kwa upande wa Morocco kwa niaba ya watu wa Saharawi. Kwa kusaini mkataba huo, Baraza la Ulaya kwa hivyo linatambua Sahara Magharibi kama jimbo la Morocco.

Kulingana na baadhi ya waangalizi , uamuzi wa mahakama ya Umoja wa Ulaya ni njia ya kuliambia Baraza kuwa liliharakia kuchukua uamuzi wa kusaini mkataba na Morocco. Hii ni mara ya kwanza kwa Umoja wa Ulaya kujibu vyema rufaa kutoka kwa kundi la Polisario Front, amblo limepongeza uamuzi ho na kusema ni "ushindi mkubwa".

Umoja wa Ulaya na Morocco, kwa upande wao, wameahidi kuendeleza ushirikiano wao wa kibiashara. "Tutachukua hatua zinazohitajika kuhakikisha mfumo wa kisheria unazingatia kuendelea na uhusiano tulivu wa kibiashara kati ya Umoja wa Ulaya na Ufalme wa Morocco," Mkuu wa Sera za Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell, na mwenzake wa Morocco, Nasser Bourita , wamesema katika taarifa ya pamoja iliyotolewa Brussels.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.