Pata taarifa kuu
MOROCCO

Morocco yamuunga mkono de Mistura kama mjumbe mpya wa UN kwa Sahara Magharibi

Maswali yameibuka kuhusu kuanza tena kwa mazungumzo kati ya Morocco na upande wa Polisario? Wakati majaribio ya kumaliza mzozo huu yameshindwa, na mazungumzo ambayo Algeria na Mauritania zimekuwa zikishiriki yamesitishwa, mjumbe mpya wa Umoja wa Mataifa wa Sahara Magharibi anatarajia kuteuliwa haraka. Morocco imetangaza kwamba iko tayari kwa mjumbe atakayeteuliwa.

Staffan de Mistura, 74, ambaye alihudumu kama mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan, Iraq na Syria, ni mwanadiplomasia mzoefu.
Staffan de Mistura, 74, ambaye alihudumu kama mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan, Iraq na Syria, ni mwanadiplomasia mzoefu. Fabrice Coffrini AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Tangu mwaka 2019 alipojiuzulu mjumbe wa Umoja wa Mataifa, Horst Köhler, raia wa Ujerumani, karibu majina kadhaa yamependekezwa na Umoja wa Mataifa. Jina la mwanadiplomasia Staffan de Mistura lilitajwa hivi karibuni na mara moja kuidhinishwa na Polisario Front.

Kwa hivyo serikali ya Morocco ilichukua muda wake, karibu miezi 6, kukubali pendekezo lililotolewa na Antonio Guterres. Balozi wa Morocco katika Umoja wa Mataifa, Omar Hilale amesema: "Makubaliano ya Morocco yanatokana na imani yake ya kudumu na kuunga kwake mkono mara kwa mara juhudi za Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kufikia suluhisho la kisiasa na kukubaliana na mzozo wa kikanda. "

Wakati Polisario, inayoungwa mkono na Algeria inataka kura ya maoni ya kujitawala chini ya mikataba ya Umoja wa Mataifa, kura ya maoni iliyopangwa tangu kusainiwa kwa kusitisha mapigano mnamo mwaka 1991, Rabat, ambayo inadhibiti asilimia 80 ya Sahara Magharibi, inapendekeza mpango wa kujitawala chini ya uhuru wake.

Staffan de Mistura, 74, ambaye alihudumu kama mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan, Iraq na Syria, ni mwanadiplomasia mzoefu. Kuteuliwa kwake kama mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Sahara Magharibi lazima sasa kuidhinishwe na wajumbe wa Baraza la Usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.