Pata taarifa kuu
MOROCCO

Morocco: Chama cha PJD chakumbwa na mgawanyiko kufuatia uchaguzi wa wabunge

Mvutano wa kisiasa na minong'ono yaripotiwa nchini Morocco baada ya uchaguzi wa Jumatano, Septemba 8. Baada ya miaka kumi katika uongozi wa serikali, chama cha Kiisilamu cha PJD kimejikuta kimeangukia pua katika uchaguzi wa wabunge, baada ya kupungukiwa viti bungeni kutoka viti 125 hadi 13 katika Baraza la Wawakilishi, kulingana na takwimu za hivi karibuni.

Chama cha PJD kinatangaza kujiuzulu kwa rais wake Saad-Eddine el-Othmani na sekretarieti kuu, Septemba 9, 2021.
Chama cha PJD kinatangaza kujiuzulu kwa rais wake Saad-Eddine el-Othmani na sekretarieti kuu, Septemba 9, 2021. AFP - FADEL SENNA
Matangazo ya kibiashara

Maafisa kadhaa wa chama cha PJD wameamua kujiuzulu katika chama hicho. Kwa sasa chama cha PJD kinakabiliwa na mgawanyiko na malumbano ya ndani. Sekretarieti kuu ya chama imekiri kuhusika na hali hiyo iliyosababisha PJD kumaliza kwenye nafasi ya 8. Alipohojiwa, baada ya mkutano, Mohammed Reda Benkhaldoun, anayehusika na uhusiano wa kimataifa katika chama cha PJD, amesema: "Kushindwa huko sio mwisho wa PJD, wala sio mwisho wa dunia. Ni malumbano tu ya ndani na yatakwisha na historia ni ndefu. Kwa hivyo tutatathmini na kurejelea upya uhusiano wetu katika masuala kadhaa. Lakini unajua, sisi ni chama chenye uaminifu, kinachotetea demokrasia, na tunawashukuru watu wote waliotupigia kura. "

Matokeo haya rasmi ya wabunge, chama cha PJD kinayachukulia kuwa ya "uzushi", "yasiyo na maana" na "yasiyokubalika". Chama hicho kimebaini kwamba kitawasilsha malalamiko yake mbele ya Mahakama ya Katiba.

Kuanguka kwa chama cha PJD kunaweza kuelezwa kwa njia kadhaa: maafisa wengi waliochaguliwa mwaka 2011 au 2016 hawakutaka kuwania chini ya tiketi ya chama cha PJD katika uchaguzi huu; mgawanyiko wa ndani kuhusiana na masuala mbalimbali kama vile kuhalalisha bangi au kuanzisha uhusiano na Israeli, kulingana na mchambuzi.

Mfalme Mohammed VI, anatarajia kumteua mtu atakayehusika na kuunda serikali, kiongozi atakayeteuliwa kutoka chama cha RNI cha Aziz Akhannouche kiliyochukuwa nafasi ya kwanza katika uchaguzi wa wabunge.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.