Pata taarifa kuu
UCHUMI-DIPLOMASIA

Bei ya mafuta yazidi kupanda nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Jamhuri ya Afrika ya Kati, nchi ya pili kwa maendeleo duni duniani kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, inakumbwa na uhaba mkubwa wa mafuta tangu mwezi Machi mwaka 2022.

Vituo vingi vimekuwa vikikumbwa na matatizo ya usambazaji kwa miezi kadhaa, na hivyo kusababisha msongamano mkubwa wa magari.
Vituo vingi vimekuwa vikikumbwa na matatizo ya usambazaji kwa miezi kadhaa, na hivyo kusababisha msongamano mkubwa wa magari. REUTERS/Luke MacGregor/Files
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumanne, serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ilitangaza ongezeko kubwa la bei ya mafuta katika nchi hii ya Afrika ya Kati, ambayo mara kwa mara inakabiliwa na matatizo ya usambazaji wa hidrokaboni.

Agizo kutoka kwa Mawaziri wa Fedha, Biashara na Nishati hupanga bei mpya za pampu zinazotumika katika eneo hilo. Petroli inapanda kutoka faranga za CFA 865 (euro 1.31) hadi faranga za CFA 1,300 (euro 1.98) kwa lita, ongezeko la zaidi ya 50%, huku dizeli ikiongezeka kwa karibu 70% na kupanda kutoka faranga za CFA 855 (euro 1.30) hadi 1,450 CFA. (Euro 2.21) kwa lita.

Bei ya Petroli imeongezeka kwa kiasi kikubwa, sawa na ongezeko la karibu 80%. Katika kituo cha mafuta, lita moja itauzwa faranga za CFA 1,150 (euro 1.75), dhidi ya faranga za CFA 645 (euro 0.98) hapo awali.

"Hali hii inatutisha," Christelle Toki, 30, mhudumu katika kituo cha mafuta cha Tradex kaskazini mwa mji mkuu, Bangui, ameliambia shirika la habari la AFP ambapo bei ya lita moja ya mafuta kwenye vituo vya mafuta ilikuwa Faranga 865 za CFA kwa miaka kadhaa.

"Nashangaa wateja sasa watanunua lita ngapi kwa bei hii, ambayo imeongezeka maradufu kabisa. Wachuuzi wa mitaani daima watakuwa kwenye ushindani na kuvutia wateja wote," amesemammoja wa wakaazi wa mji wa Bangui.

Vituo vingi vimekuwa vikikumbwa na matatizo ya usambazaji kwa miezi kadhaa, na hivyo kusababisha msongamano mkubwa wa magari.

Benki ya Dunia inakadiria kuwa 71% ya takriban wakazi milioni sita wanaishi chini ya mstari wa umaskini wa kimataifa (chini ya euro 2.15 kwa siku kwa kila mtu). Takriban nusu wanakabiliwa na uhaba wa chakula na wanategemea msaada wa kimataifa wa kibinadamu, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.