Pata taarifa kuu

Majengo ya Umoja wa Ulaya nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati yateketea kwa moto

Moto uliteketeza majengo ya ujumbe wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu, bila kusababisha hasara yoyote upande wa raia, balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati ametangaza Jumatatu.

Katika eneo la PK0, katikati mwa jiji la Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Katika eneo la PK0, katikati mwa jiji la Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Getty Images - mtcurado
Matangazo ya kibiashara

Saa nne asubuhi, majengo mengi ya Ujumbe wa Umoja wa Ulaya, yanayopatikana katikati mwa jiji la Bangui, mji mkuuwa Jamhuri ya Afrika ya Kati, yaliteketea kwa moto na moshi mweupe uliendelea kufuka kutoka kwa baadhi ya majengo, amebainisha mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP. Moto huo ulizuka "karibu usiku wa manane", kulingana na walinzi waliohojiwa na shirika la habari la AFP katika eneo la tukio.

"Majengo ya ujumbe wa EU mjini Bangui yaliteketea kwa moto jana usiku. Hakuna mtu aliyejeruhiwa", aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, Douglas Darius Carpenter, balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

"Tunafanya kazi na mamlaka za Afrika ya Kati ili kuangazia haraka sababu za tukio hilo," amesema Nabila Massrali, msemaji wa diplomasia ya Ulaya, kwenye Twitter.

"Umoja wa Ulaya utaendelea na miradi yake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kama kawaida. Moto huo haujaleta athari kwa wafanyakazi, ambao wataendelea kufanya kazi wakiwa nyumbani wakisubiri kupata jengo jipya", afisa mkuu wa EU nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati ambaye amekataa kutajwa jina ameliambia shirika la habari la AFP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.