Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

CAR: Mamlaka ya Mahakama Maalum ya Jinai yaongezwa kwa miaka 5

Mamlaka ya Mahakama Maalumu ya Jinai (CPS) nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, iliyoundwa miaka minane iliyopita kuwahukumu washtakiwa wa uhalifu dhidi ya binadamu katika nchi hii inayokabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe, imeongezwa kwa miaka mitano na Bunge la kitaifa siku ya Jumatano, mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP amebainisha.

Mamlaka ya Mahakama Maalum ya Jinai (CPS) nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, iliyoundwa miaka minane iliyopita kuwahukumu washtakiwa wa uhalifu dhidi ya binadamu katika nchi hii iliyokumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Mamlaka ya Mahakama Maalum ya Jinai (CPS) nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, iliyoundwa miaka minane iliyopita kuwahukumu washtakiwa wa uhalifu dhidi ya binadamu katika nchi hii iliyokumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Gaël Grilhot/RFI
Matangazo ya kibiashara

Muswada wa kuongeza muda wa mamlaka ya CPS umewasilishwa na Waziri wa Sheria mbele ya wabunge siku ya Jumatano, na umepitishwa wakati wa upigaji kura kufuatia mjadala bungeni, amebainisha mwandishi wa habari wa AFP.

Uamuzi huu "unaashiria utashi wa raia wa Afrika ya Kati kuendelea kuongoza vita dhidi ya kutokujali", ametangaza Waziri wa Sheria, Arnaud Djoubaye Abazene.

Pia ametoa onyo "kwa wale wanaopanga njama dhidi ya taasisi za Jamhuri, kufanya vurugu na ukatili kwa raia wasio kuwa a hatia. Lazima wajue kuwa watawajibika", amesema. CPS iliundwa mwaka wa 2015 na serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati chini ya ufadhili wa Umoja wa Mataifa lakini uchunguzi wake wa kwanza ulizinduliwa mwaka wa 2018.

Mahakama hii ya mseto, inayoundwa na mahakimu wa ndani na nje ya nchi, wakiwemo majaji na waendesha mashtaka kutoka Ufaransa, Togo, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), inahukumu uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu uliofanywa tangu mwaka 2003 nchini humo.

Kesi ya kwanza ya CPS ilifunguliwa mwezi Aprili mwaka huu kabla ya hukumu ya kwanza kutolewa mwezi Novemba. Mahakama iliwahukumu wanachama watatu wa kundi lenye silaha nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati vifungo vya kuanzia miaka 20 hadi kifungo cha maisha kwa 'uhalifu dhidi ya binadamu'.

SPC ina bajeti ya kila mwaka ya euro milioni 12, hasa zinazotolewa na Umoja wa Mataifa, EU na Marekani. Jamhuri ya Afrika ya Kati, nchi ya pili kwa maendeleo duni duniani kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, imekuwa uwanja wa vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu 2013, vifo vingi katika miaka yake ya kwanza lakini ambavyo vimepungua kwa kasi tangu 2018.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.