Pata taarifa kuu
MAPIGANO-USALAMA

Sudan Kusini: Takriban raia 166 wameuawa tangu kuanza kwa mapigano ya kikabila

Nchini Sudan Kusini, kunaripotiwa wasiwasi kuhusu ghasia katika majimbo kadhaa ya kaskazini. Afisa wa eneo hilo alitangaza Jumanne (tarehe 27 Desemba) kwamba watu 56 walipoteza maisha katika siku nne zilizopita kutokana na mapigano kikabila katika Jimbo la Jonglei.

Mtu mwenye silaha akiandamana na watu waliokimbia makazi yao katika Jimbo la Unity, kaskazini mwa Sudan Kusini, Oktoba 2015.
Mtu mwenye silaha akiandamana na watu waliokimbia makazi yao katika Jimbo la Unity, kaskazini mwa Sudan Kusini, Oktoba 2015. © Jason Patinkin/AP
Matangazo ya kibiashara

Mzozo huo ulizuka miezi kadhaa iliyopita katika kijiji cha Tonga katika jimbo la Upper Nile. Ilisababishwa na mvutano kati ya viongozi wawili wa upinzani, Johnson Olony, kutoka jamii ya Shilluk, na Simon Gatwech, kutoka jamii ya Nuer. Kisha, mapigano hayo yalienea hadi katika majimbo ya Jonglei na Unity, yanayopatikana kaskazini mwa Sudan Kusini.

Mapigano hayo amayo ni kati y wanamgambo hasimu wenye silaha, yanaathiri moja kwa moja raia papo katika eneo hilo. Takriban raia 166 wamepoteza maisha katika vita hivyo, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa katika kipindi cha miezi minne iliyopita, katika jimbo la Upper Nile kaskazini mwa Sudan Kusini. Vyanzo tofauti pia vinaelezea kuhama kwa makumi ya maelfu ya watu, wengine hata kutafuta hifadhi katika nchi jirani ya Sudan.

Wasiwasi wa kikanda

Watu waliokimbia wanaelezea ukiukwaji mwingi wa haki za binadamu: mauaji, unyanyasaji wa kijinsia, utekaji nyara, uporaji na hata uchomaji moto dhidi ya vijiji. Ukosefu huu wa usalama unatatiza upatikanaji wa misaada ya kibinadamu. Wakati hali ya katika eneo hilo ni mbaya kulingana na Umoja wa Mataifa. Waliokimbia makazi yao wanakosa chakula, vifaa vya usafi na hata huduma za afya.

Kutokana na hali hii, wito wa kusitishwa kwa mapigano unaongezeka. Katika taarifa yake Jumatatu, Desemba 26, Igad, Jumuiya ya maendeleo ya Afrika Mashariki, ilisema "inasikitishwa sana" na mapigano ya hivi majuzi. Wasiwasi pia kwa upande wa Rais wa Kenya, William Ruto, ambaye alizungumza Jumamosi Desemba 24 kwa njia ya simu na mwenzake wa Sudan Kusini, Salva Kiir, akimtaka, kwa mujibu wa taarifa yake kwa vyombo vya habari, kuchukua hatua kuleta amani nchini mwake. Na kuwezesha utoaji wa misaada ya kibinadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.