Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Sudan Kusini: Watu zaidi ya 160 wauawa katika mapigano ya makundi yenye silaha Upper Nile

Watu 166 wameuawa katika jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini na wengine zaidi ya Elfu 20 wameyakimbia makwao kufuatia mapigano kati ya makundi yenye silaha tangu mwezi Agosti.

Umoja wa Mataifa, sasa unataka serikali ya Sudan Kusini kuchunguza mzozo huo kwa kutoegemea upande wowote na kuwachukulia hatua wote waliochochea na kusababisha mauaji hayo.
Umoja wa Mataifa, sasa unataka serikali ya Sudan Kusini kuchunguza mzozo huo kwa kutoegemea upande wowote na kuwachukulia hatua wote waliochochea na kusababisha mauaji hayo. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Takwimu hizo zimetolewa na Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za binadamu, na kueleza kuwa mapigano hayo yaliyoanzia katika kijiji kimoja katika jimbo la Upper Nile, sasa yamesambaa mpaka jimboni Jongleo na Unity. 

Chanzo cha mapigano hayo, kinaelezwa kuwa mzozo wa eneo la kulisha mifungo, huku wakulima wakilalamika kuvamiwa kwa mashamba yao. 

Mbali na mauaji hayo, kumeripotiwa pia kwa visa vya wanawake na wasichana kubakwa, huku watu wengine pia wakitekwa na mali kuibiwa kwa mali ya wakaazi na watu wenye silaha. 

Umoja wa Mataifa, sasa unataka serikali ya Sudan Kusini kuchunguza mzozo huo kwa kutoegemea upande wowote na kuwachukulia hatua wote waliochochea na kusababisha mauaji hayo. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.