Pata taarifa kuu

Mwili wa mwanafunzi wa Zambia aliyeuawa nchini Ukraine kurejeshwa Zambia

Mwili wa mwanafunzi wa Zambia, aliyesajiliwa katika gereza la Urusi kabla ya kuuawa wakati wa mapigano nchini Ukraine, utarejeshwa kwa familia yake siku ya Jumapili, serikali ya Zambia imetangaza siku ya Ijumaa.

Wanajeshi wa Urusi wakiwa kwenye doria katika jiji la Mariupol, Machi 20, 2022.
Wanajeshi wa Urusi wakiwa kwenye doria katika jiji la Mariupol, Machi 20, 2022. © REUTERS/Alexander Ermochenko
Matangazo ya kibiashara

Lemekhani Nathan Nyirenda, 23 na aliye kuwa anatumikia kifungo karibu na mji wa Moscow, aliuawa mnamo mwezi wa Septemba akipigania jeshi la Urusi.

"Mwili wa Lemekhani uliwasili Moscow leo na utawasili Zambia Desemba 11," Waziri wa Mambo ya Nje wa Zambia Stanley Kakubo ameliambia Bunge la nchi hiyo.

Zambia mwezi uliopita ilidai maelezo ya haraka kutoka kwa Urusi kuhusu mazingira ya kifo chake. Wiki mbili baadaye, kundi la wanamgambo wa Urusi Wagner lilikiri kuwa lilimwajiri kijana huyo gerezani, akidai kwamba alijiunga na Wagner kwa hiari kabla ya kufa 'shujaa' huko Ukraine.

Mnamo Septemba 22, alikuwa "mmoja wa wapiganaji wa kwanza wa Urusi kuingia katika mahandaki ya adui, akionyesha ujasiri na ushujaa," mkuu wa kundi la Wagnern Evgeny Prigojine, kiongozi maarufu ambaye ni mshirika wa karibu na Vladimir Putin.

"Sheria za Urusi zinaruhusu kusamehewa kwa wafungwa katika mazingira ya operesheni maalum za kijeshi," amebaini waziri wa Zambia. "Kwa bahati mbaya, Lemekhani aliuawa," ameongeza.

Swali la fidia kwa familia kwa kifo hiki litajadiliwa "kwa wakati ufaao", ameongeza waziri huyo.

Kulingana na Zambia, kijana huyo alikuwa akisomea uhandisi wa nyuklia katika Taasisi ya Fizikia ya Uhandisi huko Moscow. Alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka tisa jela mnamo mwezi wa Aprili 2020 kwa kesi ya madawa ya kulevya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.