Pata taarifa kuu

Nyota wa mchezo wa kikapu Brittney Griner awasili Texas na kupokelewa na umati wa watu

Nchini Marekani, nyota wa mchezo wa kikapu Brittney Griner amewasili mjini Texas, baada ya serikali yake kubadilishana na mfungwa mwingine mfanyabiashara wa silaha, Viktor Bout raia wa Urusi.

Picha ya skrini ya video iliyotengenezwa na huduma za usalama za Urusi ambapo anaonekana mchezaji wa mpira wa kikapu Brittney Griner kwenye ndege ikimpeleka Abu Dhabi ambako ubadilishanaji na mfungwa mwinge wa Urusi ulifanyika, Alhamisi, Desemba 8, 2022.
Picha ya skrini ya video iliyotengenezwa na huduma za usalama za Urusi ambapo anaonekana mchezaji wa mpira wa kikapu Brittney Griner kwenye ndege ikimpeleka Abu Dhabi ambako ubadilishanaji na mfungwa mwinge wa Urusi ulifanyika, Alhamisi, Desemba 8, 2022. AP
Matangazo ya kibiashara

Griner amerejea nyumbani, miezi 10 baada ya kufungwa jela nchini Urusi, baada ya kupatikana na kosa la la kubeba, mafuta ya bangi, alipokamatwa katika uwanja wa ndege wa Moscow, mwezi Februari. 

Ikulu ya Marekani, baada ya rais Joe Biden hapo jana kutangaza kuwa, mchezaji huyo ameachiwa kufuatia mashauriano magumu na ya muda mrefu na serikali ya Urusi, na yupo katika hali nzuri na afya yake ni nzuri. 

Mashauriano hayo yalifanikiwa baada ya Marekani kukubali, kumwachia Viktor Bout mfanyabiashara wa Urusi, ambaye pia alikuwa amefungwa jela na serikali ya Washington. 

Ndege mbili za kibinafsi, moja iliyomsafirisha Bout na nyingine, Griner, zilitua mjini Abu Dhabi kutoka Moscow na Washington, kabla ya kila mfungwa, kuelendelea na safari yake. 

Wanasiasa kadhaa wa chama cha Republican wakiongozwa na rais wa zamani Donald Trump wamelaani hatua hiyo ya kubadilishana wafungwa na kwa kueleza kama kitendo cha aibu. 

Raia mwingine wa Marekani, Paul Whelan, anasalia mfungwa nchini Urusi baada ya kuhukumiwa jela miaka 16 kwa kosa la kufanya kazi la kijasusi dhidi ya serikali ya Moscow. 

Rais Vladimir Putin amesema, kuna uwezekano wa kubadilishana wafungwa na Marekani katika siku zijazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.