Pata taarifa kuu
HAKI-MAANDAMANO

Muuaji wa mwanaharakati dhidi ya ubaguzi wa rangi Chris Hani aachiliwa kwa masharti

Janusz Walus alidungwa kisu gerezani kufuatia tangazo lenye utata la kuachiliwa kwake: muuaji wa mwanaharakati dhidi ya ubaguzi wa rangi Chris Hani ameachiliwa siku ya Jumatano, serikali ya Afrika Kusini imetangaza.

Chris Hani, kiongozi wa Chama cha Kikomunisti nchini Afrika Kusini, aliuawa mwaka 1993. (Picha ya 1991)
Chris Hani, kiongozi wa Chama cha Kikomunisti nchini Afrika Kusini, aliuawa mwaka 1993. (Picha ya 1991) REUTERS/Patrick de Noirmont/Files
Matangazo ya kibiashara

"Janusz Walus ameachiliwa kwa masharti mnamo Jumatano Desemba 7," mamlaka ya magereza imesema katika taarifa.

Mwishoni mwa mwezi wa Novemba, mahakama ya juu zaidi nchini Afrika Kusini iliruhusu kuachiliwa mapema kwa Janusz Walus, 69, baada ya miaka 30 jela. Akiwa amehukumiwa kifo na kisha kifungo cha maisha, mhamiaji huyu wa Poland aliye na uhusiano na mrengo wa kulia wa Afrikaner alipaswa kuachiliwa kutoka gerezani ndani ya siku kumi.

'Walus aliruhusiwa kutoka hospitalini leo alipokuwa akitibiwa baada ya kudungwa kisu,' mamlaka ya magereza imebaini, na kuongeza kuwa hakuna shaka mfungwa huyo ni 'mtu mwenye ubaguzi' nchini.

Alidungwa kisu mnamo Novemba 29 katika gereza la Pretoria alikokuwa akitumikia kifungo chake, kitendo kilichotekelezwa na mfungwa mwingine.

Tangazo la kuachiliwa kwake lilikuwa limeamsha kumbukumbu mbaya nchini Afrika Kusini. Maandamano huko Pretoria, yaliyoitishwa na Chama cha Kikomunisti (SACP) na ANC (chama tawala), yalileta pamoja mamia ya watu wiki iliyopita.

Afisa mkuu wa tawi lenye silaha la ANC, Chris Hani, 50, aliuawa Aprili 10, 1993, katika muktadha wa mazungumzo tete na utawala wa Wazungu kwa uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia. Kifo chake cha kikatili kilizidisha mivutano ya rangi na kusababisha ghasia mbaya.

Janusz Walus alikamatwa dakika chache baada ya mauaji hayo. Katika gari lake, maafisa wa polisi waligundua silaha iliyotumiwa kwa mauaji na kwenye shati lake, kulionekana chembe za damu. Baada ya hukumu ya kifo, hukumu yake ilibadilishwa na kuwa kifungo cha maisha na ujio wa demokrasia mwaka 1994.

Alitakiwa kuachiliwa kwa masharti kwa takriban miaka 20 lakini maombi yake yote ya awali yalikataliwa.

Kifo cha Chris Hani, katika makaburi ya mashujaa wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi, huadhimishwa kila mwaka nchini Afrika Kusini. Familia yake imekuwa ikipinga vikali kuachiliwa kwa muuaji wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.