Pata taarifa kuu

Kikao cha Bunge kujadili ripoti inayomtuhumu rais Ramaphosa chaahirishwa hadi wiki ijayo

Bunge nchini Afrika Kusini, limeahirisha hadi wiki ijayo, kujadili ripoti inayomtuhumu rais Cyril Ramaphosa, kuficha mamilioni ya fedha katika makaazi yake, hatua ambayo huenda ikasababisha apigiwe kura ya kukosa imani naye.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akiondoka kwenye mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama cha African National Congress (ANC) mjini Johannesburg, Afrika Kusini, Desemba 5, 2022.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akiondoka kwenye mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama cha African National Congress (ANC) mjini Johannesburg, Afrika Kusini, Desemba 5, 2022. REUTERS - SUMAYA HISHAM
Matangazo ya kibiashara

Hii imekuja katika kipindi ambacho rais Ramaphosa ameendelea kupata shinikizo hasa kutoka kwa wanasiasa wa upinzani, ajiuzulu baada ya kile kilichoelezwa kwenye ripoti hiyo kuwa alishindwa kutoa maelezo ya kuridhisha kuhusu chanzo cha fedha hizo. 

Siku ya Jumatatu, viongozi wa chama tawala walikutana kujadili hatima ya kiongozi huyo na baada ya mashauriano ya muda mrefu walikubaliana, kupinga mswada wowote wa kumwondoa katika uongozi wa chama hicho. 

Kucheleweshwa kwa wabunge kujadili ripoti hiyo, huenda kusibadilishe maamuzi ya uongozi wa chama cha ANC, kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu Paul Mashatile. 

Uongozi wa ubunge ambao umesema, ripoti hiyo itajadiliwa Jumanne ijayo, Disemba tarehe 13, mabadiliko hayo yo muda yamefanyika ili kutoa nafasi kwa wabunge kusafiri kwenda Cape Town ili kushiriki kwenye mjadala huo. 

Ramaphosa ambaye amekanusha madia ya kuiba fedha za umma na kuzificha nyumbani kwake, na kusisitiza kuwa hatojiuzulu, amekwenda pia Mahakamani, kupinga utaratibu uliotiwa kufanya uchunguzi huo na ripoti kutolewa. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.