Pata taarifa kuu

ANC yachunguza hatima ya Rais Ramaphosa anayetishiwa kufutwa kazi

Wakuu wa chama tawala nchini Afrika Kusini ANC, wanajadiliana kuhusu hatima ya rais Cyril Ramaphosa, siku moja kabla ya bunge kujadili ripoti inayomhusisha na uvunjifu wa maadili ya uongozi, baada ya kiasi kikubwa cha fedha fedha kupatikana nyumbani kwake. 

Mapema leo, rais Ramaphosa, aliwasili katika eneo la kikao hicho, lakini hakusema neno, alitabasamu tu, akawapungia mkono wanahabari na kuondoka.
Mapema leo, rais Ramaphosa, aliwasili katika eneo la kikao hicho, lakini hakusema neno, alitabasamu tu, akawapungia mkono wanahabari na kuondoka. REUTERS - SIPHIWE SIBEKO
Matangazo ya kibiashara

Kikao cha wakuu hao wa ANC, kimekuja baada ya rais Ramaphosa, kusema hatojiuzulu, na kueleza kuwa anawaachia wakuu wa chama hicho kuamua hatima yake. 

Mapema leo, rais Ramaphosa, aliwasili katika êneo la kikao hicho, lakini hakusema neno, alitabasamu tu, akawapungia mkono wanahabari na kuondoka. 

Msemaji wa chama cha ANC Pule Mabe, amesema rais asingezewa kusalia kwenye kikao hicho kwa kuheshimu kanuni za chama hicho kuwa mshukiwa hawezi kuwa katika mkutano huo, ili kutoa nafasi kwa wakuu wa chama hicho kujadili na kuamua hatima yake kwa uhuru. 

Kumekuwa na shinikizo za kumtaka kiongozi huyo kuachia nafasi ya urais, baada ya ripoti kuonesha kuwa, alishindwa kueleza ni kwa namna gani mamilioni ya dola ilipatikana katika shamba lake huko 'Phala Phala', huku ikishukiwa kuwa ni fedha za wizi. 

Siku ya Jumanne, wabunge não watapata fursa ya kuijadili ripoti hiyo,na ripoti zinasema kuna uwezekano, wa kuwasilishwa kwa mswada wa kukosa imani, katika bunge hilo la wabunge 400 ambalo chama cha ANC kina wabunge 230. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.