Pata taarifa kuu
SIASA-HAKI

Afrika Kusini: Rais Ramaphosa "hatajiuzulu" adai msemaji wake

Msemaji wa Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, ambaye kwa sasa yuko chini ya tishio la kung'atuliwa mamlakani, anabaini kwamba rais huyo hana nia ya kujiuzulu au kuachana na siasa, amehakikisha Jumamosi hii kwa shirika la Habari la AFP. 

Rais Ramaphosa amekuwa anakabiliwa na mashitaka tangu mwezi Juni akimshutumiwa kwa kujaribu kuficha wizi huu mnano mwezi Februari 2020, ambapo dola 580,000, pesa taslimu zilizofichwa kwenye sofa ziliibiwa, na kushindwa kutoripoti tukio hilo kwa polisi wala kwa mamlaka ya kodi.
Rais Ramaphosa amekuwa anakabiliwa na mashitaka tangu mwezi Juni akimshutumiwa kwa kujaribu kuficha wizi huu mnano mwezi Februari 2020, ambapo dola 580,000, pesa taslimu zilizofichwa kwenye sofa ziliibiwa, na kushindwa kutoripoti tukio hilo kwa polisi wala kwa mamlaka ya kodi. AP - Nardus Engelbrecht
Matangazo ya kibiashara

Akihusishwa tangu Jumatano na ripoti ya bunge iliyothibitisha kwamba "alifanya" vitendo vilivyo kinyume na sheria katika kesi ya wizi katika moja ya mali yake ambapo pesa nyingi zilipatikana, rais "hatajiuzulu kwa msingi wa ripoti yenye makosa,” Vincent Magwenya ameliambia shirika la habari la AFP.

"Ni kwa maslahi ya muda mrefu na uendelevu wa demokrasia yetu ya kikatiba, mbali na urais wa Ramaphosa, kwamba ripoti hiyo yenye dosari inatiliwa mashaka, hasa inapotumiwa kama kigezo cha kumshtaki mkuu wa nchi aliye madarakani," ameeleza msemaji wake.

Rais Ramaphosa amekuwa anakabiliwa na mashitaka tangu mwezi Juni akimshutumiwa kwa kujaribu kuficha wizi huu mnano mwezi Februari 2020, ambapo dola 580,000, pesa taslimu zilizofichwa kwenye sofa ziliibiwa, na kushindwa kutoripoti tukio hilo kwa polisi wala kwa mamlaka ya kodi. Malalamiko haya bado hayajasababisha kufunguliwa mashtaka yoyote na uchunguzi wa polisi unaendelea.

ANC, chama cha Cyril Ramaphosa madarakani tangu kuanguka kwa ubaguzi wa rangi, kitakutana Desemba 16 ili kumteua rais wake ajaye mwaka 2024, ikiwa hata hivyo chama, kinachozidi kushindana, kitashinda uchaguzi wa wabunge. Mkuu wa nchi "alitilia maanani ujumbe usio na shaka uliotoka kwa matawi ya chama tawala ambacho kilimteua kwa muhula wa pili kuwa kiongozi wa ANC", anasema msemaji wake. "Rais amekubali kwa unyenyekevu, uangalifu mkubwa na kujitolea , wito huu wa kuendelea kutoa huduma kwa chama chake, ANC, na kwa raia wa Afrika Kusini”.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.